Pata taarifa kuu
DRC-WAASI-MAUAJI-USALAMA

Watu wengine tisa wauawa baada ya kushambuliwa na watu wenye silaha Wilayani Beni

Watu wenye silaha, wamewauwa watu tisa, katika  mauaji ya hivi karibuni kutokea katika Wilaya ya Beni, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na kuendelea kuzua wasiwasi miongoni mwa raia kuhusu usalama wao.

Raia wa mji wa Beni  akiondoka nyumbani kwake kwa hofu ya kushambuliwa na watu wenye silaha
Raia wa mji wa Beni akiondoka nyumbani kwake kwa hofu ya kushambuliwa na watu wenye silaha AFP PHOTO / LIONEL HEALING
Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema kuwa, watu hao waliuawa kwa kukatwa mapanga katika kijiji cha Manzati, Kilomita 25 kutoka mji wa Eringeti katika wilaya hiyo.

Mwakilishi wa Gavana katika eneo hilo, amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo yaliyotokea Jumatano asubuhi.

“Kijiji cha Manzati kilishambuliwa na watu wenye silaha, nyakati za asububi na  watu wameuawa na wengine kuamua kuondoka,” alisema.

Hali hii imezua wasiwasi mkubwa, na watu zaidi ya 200 wamekimbilia katika mji wa Eringeti kwa hofu kuwa wanaweza kushambuliwa tena.

“Nimeamua kukimbia baada ya kushuhudia mauaji, moyo wangu umechoka sana, watu wengi wamekimbia,” alisema mmoja wa watu walioamua kukimbia.

Mashirika ya kiraia, yanasema kuwa, watu zaidi ya 40,000 wameyakimbia makwao kutokana na ukosefu wa usalama unaoendelea kushuhudiwa katika wilaya hiyo.

Tangu mwezi Oktoba mwaka 2019, mamia ya raia wamepoteza maisha, huku waasi wa ADF Nalu wakishtumiwa kuhusika na ukosefu wa usalama.

Licha ya serikali kupitia jeshi la FARDC kutangaza kushirikiana na lile la Umoja wa Mataifa MONUSCO kupambana na waasii hao, mauaji yameendelea kushuhudiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.