Pata taarifa kuu
AFRIKA-UCHAGUZI-SIASA-USALAMA

Uchaguzi Mkuu kufanyika mwaka 2020 katika baadhi ya nchi za Afrika

Mataifa mbalimbali yanatarajiwa kuwa na Uchaguzi Mkuu mwaka 2020, ambao utaweka katika mizani, demokrasia katika bara la Afrika.

Moja ya vituo vya kupigia Burundi.
Moja ya vituo vya kupigia Burundi. Photo:Esdras Ndikumana/AFP
Matangazo ya kibiashara

Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, Tanzania, Burundi na Ethiopia yanajiandaa katika uchaguzi muhimu utakaobadilisha mustakabali wa nchi hizo. Nchini Burundi, uchaguzi wa urais na wabunge utafanyika mwezi Mei.

Rais Pierre Nkurunziza ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 2005, alitangaza mwaka uliopita kuwa hatawania tena urais. Hata hivyo, wanasiasa wa upinzani wanasema hawaamini maneno ya Nkurunziza kwa sababu mwaka 2015 aliamua kuwania urais kwa muhula wa tatu, kinyume cha katiba ya nchi hiyo.

Mwezi Oktoba, nchini Tanzania, rais John Magufuli anatarajiwa kutetea wadhifa wake, kuwania uongozi kwa muhula wa mwisho.

Uchaguzi huo ambao unatarajiwa kufanyika mwezi Oktoba, utakuja wakati wanasiasa wa upinzani wakidai kuwa uongozi wa sasa umeweka mazingira magumu ya kufanya mikutano ya kisiasa.

Mwanasiasa wa upinzani Tundi Lissu ambaye yuko Ubelgji alikoenda miaka miwili iliyopita, tayari iwapo chama chake cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, kitampa tiketi, atawania nafasi hiyo.

Mataifa mengine ambayo yanatarajiwa kuwa na uchaguzi huu ni pamoja na Ghana, Guinea, Cote d'Ivoire, Niger, Togo na Ushelisheli.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.