Pata taarifa kuu
BURUNDI-SIASA-USALAMA

Kauli ya Rais Nkurunziza yatia mashaka upinzani

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza kwa mara nyingine siku ya Alhamisi, amesisitiza kuwa hana nia ya kuwania urais, wakati wa Uchaguzi Mkuu mwaka 2020.

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza, Juni 7, 2018.
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza, Juni 7, 2018. REUTERS/Evrard Ngendakumana
Matangazo ya kibiashara

Ametoa kauli hiyo katika mkutano na wanahabari licha ya wapinzani wake kusema kuwa hawaamini iwapo hatawania tena wadhifa huo.

Nkurunziza amesema anataka kupumzika na kuwapa nafasi watu wengine wafanye kazi kwa sababu wanao uwezo huo.

“Sipendi vyeo au hata kuwa Waziri Mkuu, acha wengine waje ili waongoze, katiba yetu ipo wazi kabisa kuhusu hili,” alisema.

Mwaka 2015, Nkurunziza aliwania urais kwa muhula wa tatu, suala ambalo lilizua vurugu nchini na kusabisha maafa pamoja na maelfu ya watu kuondoka nchini humo, wakiwemo wapinzani ambao wengi bado wanaishi nje ya nchi.

Kuhusu usalama, rais huyo, ameishtumu Rwanda kwa kuishambulia nchi yake hivi karibuni baada ya kukabiliana na wanajeshi wa taifa lake, katika Msitu wa Kibira, wilayani Mabayi, katika mkoa wa Cibitoke, Kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.