Pata taarifa kuu
ALGERIA-SIASA-USALAMA

Maswali yaibuka baada ya kifo cha Jenerali Gaïd Salah Algeria

Nchini Algeria, Jenerali Ahmed Gaïd Salah ndiye mtu ambaye alikuwa amefungua mvutano na waandamanaji kwa kujaribu kuweka masharti dhidi ya maandamano yao.

Maandamano katika mitaa ya Algiers, Machi 8, 2019. (picha ya kumbukumbu)
Maandamano katika mitaa ya Algiers, Machi 8, 2019. (picha ya kumbukumbu) RYAD KRAMDI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Wengi wanajiuliza iwapo kifo chake kitabadilisha mambo mengi nchini Algeria.

Mrithi wake ataendeleza jukulumu lake, kwa kukabiliana na waandamanaji na ktumia mkono wa chuma nchini humo kama alivyofanya mtangulizi wake? Yopte hayo ni maswali ambayo wengi nchini Algeria wanajiuliza.

Jenerali Ahmed Gaid Salah, ambaye alikuwa mkuu wa majeshi nchini Algeria, alipata umaarufu mkubwa baada ya kumkinaisha rais wa zamani Abdelaziz Bouteflika kujiuzulu.

Baada ya kujiuzulu kwa Bouteflika mwezi Aprili, Jenerali Salah alichukua madaraka kwa muda katika kipindi cha mpito.

Jenerali Salah, mmoja wa wapiganaji wa zamani wa nchi hiyo wakati wa vita vya uhuru kati ya mwaka 1954 hadi 1962, dhidi ya Wafaransa, alifariki dunia Jumatatu asubuhi wiki hii baada ya kupata mshtuko wa moyo.

Pamoja na kukumbukwa kumshinikiza rais wa zamani Bouteflika kuachia madaraka, alishirilki pakubwa kuandaa Uchaguizi wa urais uliofanyika mwezi huu, licha ya maandamano makubwa ya kupinga uchaguzi huo.

Serikali ya Algeria imetangaza siku tatu za maombolezo na tayari Jenerali Said Chengriha ametangazwa kuwa mkuu mpya wa Majeshi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.