Pata taarifa kuu

Somaliland kushiriki uchaguzi wa urais mwezi Novemba mwaka huu

Wananchi wa Somaliland, jimbo lenye utawala wake wa ndani lililojitenga na Somalia, watafanya uchaguzi wa urais tarehe 13 mwezi wa Novemba 2024, kwa mujibu wa tume ya kitaifa ya uchaguzi, orodha ya uchaguzi huo imechapishwa Jumatatu ya wiki hii.

Uchaguzi wa mwaka huu unakuja baada ya rais Muse Bihi Abdi kuongeza muda wake wa kuhudumu kwa miaka 2.
Uchaguzi wa mwaka huu unakuja baada ya rais Muse Bihi Abdi kuongeza muda wake wa kuhudumu kwa miaka 2. AFP - EDUARDO SOTERAS
Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi wa mwaka huu unakuja baada ya rais Muse Bihi Abdi kuongeza muda wake wa kuhudumu kwa miaka 2, hatua iliyofuatia mzozo wa kujitenga huko Las Anod, mashariki mwa nchi.

Muse Bihi, Rais wa Somaliland.
Muse Bihi, Rais wa Somaliland. © Malak Harb / AP

Somaliland ilijitenga na Somalia mwaka 1991 na bado inatafuta kutambuliwa kimataifa.

Mwanzoni mwa mwaka huu, Rais Muse Bihi Abdi alijaribu kutathmini kiwango cha mshikamano wa taifa lake, kwa kusaini mkataba wa maelewano na Ethiopia, hatua ambayo ilipokelewa vibaya na utawala wa Mogadishu.

Soma piaSomalia: Puntland na Somaliland zakataa kufunga balozi ndogo za Ethiopia

Lakini upinzani unamshutumu rais huyo kwa kutaka kurejesha mambo ambayo baadhi ya wanasiasa wanasema yalilenga kudhoofisha mshikamano wa nchi.

Wadadisi wa mambo wanasema ili kufanikisha uchaguzi wa Novemba 13 mwaka huu, Tume ya Uchaguzi itatakiwa kujumuisha vyama vya siasa na asasi za kiraia ili kuzuia ushindani wowote wa kura.

Na Ruben Lukumbuka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.