Pata taarifa kuu
ALGERIA-SIASA-UCHAGUZI

Maandamano yaendelea licha ya ushindi wa Abdelmadjid Tebboune Algeria

Abdelmadjid Tebboune ameibuka mshindi katika katika duru ya kwanza katika uchaguzi wa urais uliofanyika Alhamisi wiki hii nchini Algeria. Hata hivyo uchaguzi huo ulisusiwa na idadi kubwa ya raia wa Algeria. Kiwango cha ushiriki kilifikia 39.9%.

Kadi ya mgombea aliyeshinda uchaguzi Abdelmadjid Tebboune katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais nchini Algeria, Desemba 12, 2019.
Kadi ya mgombea aliyeshinda uchaguzi Abdelmadjid Tebboune katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais nchini Algeria, Desemba 12, 2019. RYAD KRAMDI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Vuguvugu la Hirak lilikuwa limetolea wito wananchi wa Algeria kususiauchaguzi huo. Leo Ijumaa himamia ya maelfu ya watu wamefurrika katika mitaa ya miji mbalimbali ya nchi hiyo kupinga uchaguzi huo.

Vigivigi hilo lililoanzishwa tangu mwezi Februari mwaka huu limeapa kuendelea na maandamano hayo kupinga uchaguzi huo na ushindi huo.

Katika mji mkuu Algiers, tayari waandamanaji wamemiminika mitaani, huku wakiimba nyimbo zinazoshtumu uchaguzi huo kwamba uligubikwa na wizi.

Algeria imeendelea kukumbwa na maandamano, huku waandamanaji wakitaka kwanza kuondolewa kwa wagombea na viongozi waliokuwa chini ya utawala wa rais Abdelazizi Bouteflika

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.