Pata taarifa kuu
KENYA-WALIMU-AFRIKA-ELIMU

Walimu Wakuu wa Shule za Sekondari barani Afrika wakutana Mombasa, Kenya

Kongamano la 10 linawakutanisha Walimu Wakuu wa Shule za Sekondari barani Afrika, mjini Mombasa Pwani ya Kenya,  kujadili masuala mbalimbali kuhusu namna ya kuimarisha sekta ya elimu.

Rais Uhuru Kenyatta akisalimiana na Walimu Wakuu kutoka barani Afrika wanaokongamana mjini Mombasa nchini Kenya Agosti 07 2018
Rais Uhuru Kenyatta akisalimiana na Walimu Wakuu kutoka barani Afrika wanaokongamana mjini Mombasa nchini Kenya Agosti 07 2018 PSCU
Matangazo ya kibiashara

Rais Uhuru Kenyatta alifungua kongamano hilo siku ya Jumanne na kutoa wito kwa Wakuu hao wa Shule za Sekondari barani Afrika, kuhakikisha kuwa wanawahimiza wanafunzi kutambua umuhimu wa Umoja wa Afrika na kujitambua kama Waafrika.

Aidha rais Kenyatta, ameahidi kuwashawishi viongozi wenzake kutoka mataifa mbalimbali ya  Afrika, kuutambua muungano huo wa Walimu Wakuu ili uwe mwangalizi katika mikutano ya Umoja wa Afrika.

Mbali na viongozi hao wa Shule za Sekondari, kongamano hilo pia linawakutanisha watalaam wa elimu kujadiliana pamoja kuhusu namna ya kuimarisha sekta hiyo nyeti la elimu na usimamamizi bora wa Shule.

Kenya inatarajiwa kukabidhiwa uongozi wa muungano huo ambao sasa utaongozwa na Indimuli Kahi, rais wa Walimu Wakuu nchini humo.

Kongamano hilo linamalizika siku ya Ijumaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.