Pata taarifa kuu
ZIMBABWE-SIASA-USALAMA

Aliyemtimua Mugabe madarakani ateuliwa kuwa makamu wa rais

Rais mpya ya Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amewateua makamu wake wawili. Jenerali Constantino Chiwenga na Waziri wa zamani Kembo Mohadi wote wameapishwa Alhamisi hii asubuhi Desemba 28.

Constantino Chiwenga lors de sa nomination en tant que vice-président du Zimbabwe, le 28 décembre 2017.
Constantino Chiwenga lors de sa nomination en tant que vice-président du Zimbabwe, le 28 décembre 2017. AFP/Wilfred Kajese
Matangazo ya kibiashara

Uteuzii wao ulikuwa ukitarajiwa wiki iliyopita wakati ambapo wawili hao waliteuliwa kuwa manaibu wa kiongozi wa chama tawala, Zanu-PF.

Uteuzi wa Chiwenga katika serikali unaonesha dhahiri jinsi gani serikali mpya iko mikononi mwa jeshi.

Jenerali Constantino Chiwenga aliongoza jeshi kumtimua mamlakani aliyekuwa rais wa taifa hilo Robert Mugabe mnamo mwezi Novemba.

Alistaafu hivi karibuni na kuwa naibu kiongozi wa chama tawala cha Zanu-Pf mnamo Disemba 2.

Rais mpya Emmerson Mnangagwa alichukua hatamu ya uongozi baada ya jeshi kuingilia kati tarehe 15 mwezi Novemba kufuatia mgogoro wa kumrithi Robert Mugabe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.