Pata taarifa kuu
ZIMBABWE-UCHUMI

Wazungu warudishiwa mashamba yao Zimbabwe

Serikali ya Zimbabwe kupitia Waziri wake mpya wa kilimo, imeamuru kuridishwa kwa mashamba yaliyokua yakimilikiwa na wakulima Wazungu, ambao walinyang'anywa wakati wa utawala wa Mugabe na kupewa raia wa Zimbabwe.

Sarafu ya Zimbabwe imeanguka kutokana na hali mbaya ya kiuchumi.
Sarafu ya Zimbabwe imeanguka kutokana na hali mbaya ya kiuchumi. REUTERS/Philimon Bulawayo
Matangazo ya kibiashara

"Wote ambao wamewekwa kinyume cha sheria katika mashamba ambayo si mali yao wanapaswa kuyarudisha haraka iwezekanavyo," alisema Perence Shiri, Waziri mpya wa Kilimo wa Zimbabwe siku ya Alhamisi.

Waziri Shiri alisema kuwa wale ambao wana vibali rasmi wataruhusiwa kuendelea kulima katika mashamba hayo ili kuhakikisha uzalishaji.

Shiri alisema kuwa hatua hiyo inalenga kukuza kilimo kwa ajili ya uchumi wa nchi hiyo ambao unaendelea kudorora kila kukicha.

"Ikiwa tunataka kufanikisha malengo yaliyowekwa na serikali na kutumia kilimo kama nguzo ya uchumi, lazima tuhakikishe urasibu mzuri wa kilimo," waziri Shiri aliongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.