Pata taarifa kuu
UFARANSA-MALI-MACRON-USHIRIKIANO

Emmanuel Macron kuzuru Mali kukutana na askari wa Barkhane

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anatarajiwa Alhamisi hii kuzuru Mali. Katika ziara yake ya kwanza barani Afrika tangu kuchaguliwa kwake, Emmanuel Macron atakutana na kikosi cha askari wa Ufaransa wa operesheni Barkhane.

Emmanuel Macron aelekea Mali kukutana na kikosi cha Barkhane.
Emmanuel Macron aelekea Mali kukutana na kikosi cha Barkhane. REUTERS/Yoan Valat/Pool
Matangazo ya kibiashara

Kwa sababu za kiusalama, maelezo ya ziara ya Emmanuel Macron nchini Mali hayajulikani. Lakini hatua muhimuya itakuwa katika mji wa Gao, mji mkuu wa kaskazini mwa Mali. Katika eneo hilo ndipo kunapatikana idadi kubwa ya askari wa Ufaransa wa operesheniya Barkhane.

Askari wa Operesheni Barkhane wanakadiriwa 4000 katika nchi tano za ukanda wa Sahel. Kikosi hiki kiliundwa mwaka 2013, baada ya askari wa Ufaransa kuingilia kijeshi kuzuia wanamgambo wa kiislamu waliokua wakisonga mbele katika maeneo mbalimbali ya kivita kusini mwa Mali. Hata hivyo wanamgambo hao bado wanaendelea kuhuhumu raia nchini humo, na askari wa Ufaransa wanaendelea na mapambano dhidi ya makundi hayo. Lengo la rais mpya wa Ufaransa ni kukutana na askari wa Ufaransakama amiri jeshi mkuu.

Emmanuel Macron pia atakutana na mwenzake wa Mali Ibrahim Boubacar Keïta.

Baraza la kitaifa la vijana nchini Mali limemuomba rais Emmanuel Macron kuhakikisha kwamba vijana Waafrika wanafikiriwa, huku Afrika kwa ujumla ikiwezeshwa kwa uadilifu, utu, na heshima.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.