Pata taarifa kuu
UFARANSA-SERIKALI MPYA

Serikali Mpya nchini Ufaransa yatangazwa

Rais mpya wa Ufaransa Emmanuel Macron ameteua Baraza lake la kwanza la Mawaziri siku kadhaa baada ya kuapishwa na kumteua Waziri Mkuu Edouard Philippe. Baraza hilo limetajwa kuwa na mawaziri wengi wapya wakiwemo kutoka mrengo wa kushoto na wakulia, pamoja na mashirika ya kiraia

Emmanuel Macron,rais mteule wa Ufaransa
Emmanuel Macron,rais mteule wa Ufaransa 路透社
Matangazo ya kibiashara

Macron amemtaja mwanasiasa mkongwe kutoka chama cha Kisosholisti Jean-Yves Le Drian mwenye umri wa maiak 69, kuwa Waziri wa Mambo ya nje. Le Drian alikuwa waziri wa Ulinzi katika serikali ya Francois Hollande.

Mwanasiasa huyo wa siku nyingi, alihudumu kama Waziri wa Ulinzi katika serikali iliyopita ya rais Francois Hollande.

Bi. Sylie Goulard ambaye amekuwa Mbunge wa  bunge la Umoja wa Ulaya kutoka vuguvugu la En Marche, ameteuliwa kuwa Waziri wa Ulinzi.

Waziri wa zamani wa chakula, Kilimo na Uvuvi Bruno Le Maire kutoka chama cha Republican ndio Waziri mpya wa Fedha.

Mawaziri wengine muhimu waliotajwa ni pamoja na Meya wa jiji la Lyon Gerard Collomb, ambaye ni Waziri wa Mambo ya ndani.

Mgombea wa zamani wa urais mwaka 2002, 20007 na 2012, Francois Bayrou ndio Waziri mpya wa maswala ya sheria.

Laura Fessel bingwa wa dunia na olympiki wa michozo ya mapanga, ameteuliwa kuwa waziri wa michezo.

Kikao cha kwanza cha baraza la mawaziri kimepangwa kufanyika kesho majira ya saa tano mchana za huko Paris ambapo rais Emmanuel Macron anataraji kutoa muelekeo mpana wa serikali yake katika kipindi cha miaka mitano.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.