Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE-USALAMA

Askari wa vikosi maalum vya jeshi la Cote d'Ivoire waingia mitaani

Askari wa vikosi maalum vya jeshi nchini Cote d'Ivoire wameingia mitaani na kuanza kufyatua risasi hovyo Jumanne hii mapema asubuhi katika mji wa Adiéké, eneo lililo kusini mwa nchi, karibu na mpaka na Ghana.

Askari wa vikosi maalum vya Cote d'Ivoire katika mji wa Adiaké, karibu na mpaka na Ghana, Septemba 24, 2012.
Askari wa vikosi maalum vya Cote d'Ivoire katika mji wa Adiaké, karibu na mpaka na Ghana, Septemba 24, 2012. AFP PHOTO/ SIA KAMBOU
Matangazo ya kibiashara

Sababu ya uasi huo ni malipo ya mishahara. Tukio hili linatokea mwezi mmoja tu baada ya lile la askari walioasi wakidai malipo ya mishahara yao katika mji wa Bouake.

Kwa mujibu wa mkaazi mmoja wa mji wa Adiaké aliyehojiwa na BBC, milio ya kwanza ilisikika karibu saa 1:00 asubuhi na kila mtu alilazimika kusalia nyumbani.

"Shule, maduka na makampuni vilifungwa," shahidi pia amearifu.

Askari wa ikosi maalum vya jeshi la Cote d'Ivoire, ambao ni nadra kuonekana hadharani inadaiwa kuwa ni waaminifu kwa serikali.

"Uasi huo umewashangaza wengi. Askari wa vikosi maalum hawajawahi kujiunga na uasi ulioendeshwa na idadi kubwa ya jeshi ambao walidai malipo ya marupurupu yao mwezi uliopita," kimesema chanzo hicho.

Vyombo vya habari nchini Cote d'Ivoire vimebaini kuwa askari wa vikosi maalum wanamshtumu kiongozi wao, Jenerali Lassina Doumbia, kushikilia marupurupu yao ya kila siku kwa kikosi cha ulinzi wa mpaka karibu na Ghana.

Viongozi wa kijeshi na serikali bado wahajeleza chochote kuhusu hali hiyo. Hata hivyo msemaji wa serikali ya Cote d'Ivoire amesema haina taarifa yoyote kuhusu tukio hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.