Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE-USALAMA

Milio ya risasi yasikika katika miji mbalimbali Cote d'Ivoire

Milio ya risasi imekuwa ikisikika karibu na kambi kubwa ya wanajeshi katika mji wa Bouake, mji wa pili kwa ukubwa nchini Cote d'Ivoire. Ripoti zinasema hali hii imeshuhudiwa baada ya vituo viwili vya polisi kushambuliwa na silaha kutoweka katika mji huo.

Gari la polisi katika mji wa Bouake, Januari 6, 2017.
Gari la polisi katika mji wa Bouake, Januari 6, 2017. STR / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mwanajeshi mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe ameliambia Shirika la Habari la Ufaransa AFP, kuwa wapiganaji wa zamani ambao kwa sasa wanahudumu katika jeshi la serikali ndio wanaohusika na tukio hili.

Ameeleza kuwa wapiganaji hao wa zamani wanataka kulipwa marupuru ya Dola za Marekani elfu nane kila mmoja, kupewa nyumba na kupandishwa vyeo.

Ijumaa hii mjini Bwake, shughuli zimekwama, hakuna maduka yaliyofunguliwa wala wanafunzi kwenda shule.

Ikumbukwe kuwa wapinagaji hawa zamani walioshiriki katika mapigamo ya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2002, walijaribu kumpindua kiongozi wa wakati huo Laurant Gbabgo lakini hawakufanikiwa.

Pamoja na hilo, mwaka 2010 baada ya kuzuka kwa mzozo wa kisiasa nchini humo kati ya Gbagbo na rais wa sasa Alassane Ouattara, wapiganaji hao walimuunga mkono Ouattara na kumsaidia kuingia madarakani.

Wadadisi wa mambo wanasema, hali hii ya wanajeshi hao , inamaanisha kuwa kuna ahadi ambazo rais Ouattara hakuwatimizia baada ya kuingia madarakani na ndio chanzo cha hali hii ya sintofahamu.

Serikali imewaambia wanajeshi kusalia watulivu inaposhughulikia suala hili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.