Nigeria: watu 17 wauawa Yobe
Watu 17 wamepoteza maisha baada ya kutokea kwa mashambulizi matatu ya kujitoa mhanga katika jimbo la Yobe.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Mashambulizi hayo yalitokea huku kundi la Boko Haram likitoa mkanda mpya wa video na kudai kuwa kiongozi wao Abubakar Shekau bado ni mzima na anaedelea kuwaongoza.
Haya ndio mashambulizi mabya kuwahi kutokea katika jimbo hilo na hasa mjini Damaturu katika siku za hivi karibuni.
Shambulizi la kwanza lilitokea katika gala ndogo la chakula na kusabaisha vifo vya watu kadhaa, na lingine kutokea katika msikiti na lingine kutokea katika boma la mifugo nje ya mji huo.
Gavana wa jimbo hilo Ibrahim Gaidam ameshtumu mashambulizi hayo na kutaka serikali kuimarsiha usalama ili kukabiliana na Boko Haram.
Rais Muhamadu Buhari amelipa jeshi la nchi hiyo hadi mwezi Novemba kulitokomeza kabisa kundi hilo la Islamic State Afrika Magharibi.