Pata taarifa kuu
NIGERIA-BOKO HARAM-USALAMA

Kiongozi wa Boko Haram asema bado yuko hai

Abubakar Shekau ametoa ushahidi kuwa bado yuko hai. Katika ujumbe wa sauti ambao wataalam wanaamini kuwa ni sauti yake, kiongozi wa kundi la zamani la Boko Haram ametoa ujumbe huo kwa dunia na hasa kwa Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari.

Video ya propaganda ya Boko Haram ikimuonyesha kiongozi wake Abubakar Shekau, Januari 20, 2015.
Video ya propaganda ya Boko Haram ikimuonyesha kiongozi wake Abubakar Shekau, Januari 20, 2015. AFP PHOTO / BOKO HARAM
Matangazo ya kibiashara

" Niko hai, tuko hai. Hii ni sauti yangu. Ni mimi Shekau ", amesema Shekau. Baada ya miezi kadhaa ya ukimya, Abubakar Shekau amesema ili aweze kusikika kuwa bado yuko hai. Katika ujumbe wa sauti uliyorushwa hewani katika mitandao ya kijamii mwishoni mwa wiki hii, kiongozi wa kundi la Islamic State Afrika Magharibi anataka kuzima uvumi uliyozagaa ulimwengu mzima kuwa ameshafariki.

Video yake ya mwisho ilikuwa mwezi Februari mwaka huu. Na mpaka katika ujumbe wake wa mwezi uliopita, kutoonekana kwake katika mawasiliano ya hivi karibuni ya kundi hili la zamani la Boko Haram kumesababisha uvumi kunea duniani kote kuwa Abubakar Shekau katoweka. Katika lugha za Kihausa na Kiarabu, Abubakar Shekau amemshambulia kwa maneno Rais Muhammadu Buhari, akichukulia ahadi zake za ushindi katika muda wa miezi mitatu.

Hakuna dalili ya mahali na tarehe maalum viliyowekwa katika mawasiliano haya ya dakika 25. Hata hivyo, skimssnishs mkataba kati ya François Hollande na Muhammadu Buhari, nidhahiri kuwa ujumbe huu ni wa hivi karibuni.

Rais wa Nigeria, wiki iliyopita, alifanya ziara rasmi mjini Paris. Akimaanisha katika ujumbe kwa ndugu zake wanaoshikiliwa katika jela mbalimbali nchini Nigeria, Abubakar Shekau hakumjibu Rais wa Nigeria kuhusu uwezekano wa kubadilishana baadhi ya wafungwa wake dhidi ya wasichana wote waliotekwa nyara katika shule ya upili ya mji wa Chibok.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.