Pata taarifa kuu
ICC-GBAGBO-SHERIA-HAKI

ICC: ombi la kuachiliwa huru la Laurent Gbagbo lafutiliwa mbali

Rais wa zamani wa Côte d’Ivoire Laurent Gbagbo itabidi asubiri katika jela la mjini Hague angalau hadi mwezi Novemba, siku iliyopangwa kwa kesi yake.

Laurent Gbagbo, Februari 2013 Hague.
Laurent Gbagbo, Februari 2013 Hague. AFP PHOTO/ POOL/ MICHAEL KOOREN
Matangazo ya kibiashara

Ombi la kuachiliwa huru la Rais wa zamani limekataliwa lJumanne asubuhi wiki hii na majaji wa Mahakama ya kimataifa ya uhalifu(ICC). Wanasheria wa Rais wa zamani mwenye umri wa miaka 70 wamekua wakiomba mteja wao achiliwe huru kwa muda kutokana na afya yake.

Rais huyo wa zamani wa Côte d’Ivoire atavumilia na kuendelea kuishi katika jela la mjini Hague kwa kusubiri hatima yake mwezi Novemba. Ombi la kuachiliwa huru kwa muda la Laurent Gbagbo limekataliwa na majaji wa Mahakama ya kimataifa ya uhalifu. Wanasheria wake wamesema kuwa uamuzi uliyochukuliwa dhidi ya mteja wao ni wa kisiasa. " Tunaamini kwamba ICC iko kwenye mtazamo wa kisiasa! Umazi huu ni wa kutaka kumuweka mteja wetu kando kabisa na siasa. Nadhani kwamba mtazamo huo wa kisiasa sio siri tena. Mambo yako wazi! ", wakili Toussaint Dako ameiambia RFI.

Kwa upande wake, ICC imehakikisha kwamba haikushini kimaamuzi wala maamuzi yake hayahusiani na hali ya ndani ya siasa za nchi. " Hakuna masuala ya kisiasa yaliyozingatiwa katika maamuzi ya majaji wa ICC. Kama ilivyo sasa, majaji wamezingatia haja ya kumbakiza Laurent Gbagbo chini ya ulinzi akisubiri ufunguzi wa kesi yake. Masuala yanayohusiana na sera ya taifa ni mambo ya mamlaka ya kitaifa, si ICC ", amejibu Fadi Abdallah, msemaji wa ICC

Kesi ya Rais wa zamani wa Côte d’Ivoire itaanzishwa mwezi Novemba mwaka huu mjini The Hague.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.