Pata taarifa kuu
CAR-UN-TUHUMA-HAKI

CAR: UN yamteua Onanga-Anyanga kwenye uongozi wa Minusca

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa amemteuwa Parfait Onanga-Anyanga, raia wa Gabon, kwenye uongozi wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, baada ya kujiuzulu kwa Babacar Gaye kufuatia kashafa za ngono zinazokisiwa kutekelezwa na walinda amani wa Munisca.

Parfait Onanga-Anyanga, aliye kuwa hivi karibuni mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Burundi, ameteuliwa kuwa mkuu wa Minusca baada ya kujiuzulu kwa Babacar Gaye, raia wa Senegal.
Parfait Onanga-Anyanga, aliye kuwa hivi karibuni mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Burundi, ameteuliwa kuwa mkuu wa Minusca baada ya kujiuzulu kwa Babacar Gaye, raia wa Senegal. UN Photo/Loey Felipe
Matangazo ya kibiashara

Ban Ki-moon pia ameongeza kutilia mkazo sera zake za kutovumilia makosa yanayotuhumiwa vikosi vya majeshi ya Umoja wa Mataifa, hususan kashfa za ngono, wakati ambapo shutuma za uhalifu wa kijinsia dhidi ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa zimekua nyingi miaka ya hivi karibuni.

Ban Ki-moon amefahamisha wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa chaguo lake la kumteua Perfect Onanga-Anyanga kwenye nafasi ya Babacar Gaye, raia kutoka Senegal, wakati wa mkutano wa faragha, ambapo ameeleza uamuzi wake wa kumuomba Babakar Gaye kujiuzulu. Kuondoka kwake kumekuja baada ya mfululizo wa tuhuma za unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya watoto uliofanywa na walinda amani wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Parfait Onanga-Anyanga alikua hivi karibunimjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Burundi. Ameteuliwa kwenye uongozi wa ujumbe wa Umoja wa Mataida nchini Jamhuri ya afrika ya kati (Minusca) wakati amabpo ujumbe huo unakabiliwa na tuhuma 57 za makosa, ikiwa ni pamoja na 11 zinazohusu unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.