Pata taarifa kuu
CAR-SELEKA-ANTIBALAKA-Machafuko-Usalama

CAR: Afisa wa kikosi cha UN auawa

Afisa wa kikosi cha wanajeshi wa Umoja wa Mataifa kutoka Pakistan ameuawa Alhamisi jioni wiki hii na wengine tisa wamejeruhiwa katika shambulio la kuvizia karibu na mji wa Bangui, nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Kikosi cha wanajeshi wa Umoja wa Mataifa kikipiga doria katika mitaa ya mji wa Bangui, kufuatia kuzuka kwa machafuko Ijumatano Oktoba 8 mwaka 2014.
Kikosi cha wanajeshi wa Umoja wa Mataifa kikipiga doria katika mitaa ya mji wa Bangui, kufuatia kuzuka kwa machafuko Ijumatano Oktoba 8 mwaka 2014. PACOME PABAMDJI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo limetokea siku moja baada ya taifa hilo kuingia katika mgogoro wa kisiasa baada ya wanamgambo wa kikristo wa Anti-balaka kumtaka rais wa taifa hilo, Catherine Samba-Panza ajiuzulu.

Ni kwa mara ya kwanza kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati Minusca kinashambuliwa tangu kilipowasili nchini humo Septemba 15. Wanajeshi wa kikosi hicho wameshambuliwa na watu wenye silaha wakati walikua wakipiga doria katika wilaya ya PK11 kando ya mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Bangui.

“ Alhamisi jioni wiki hii, kikosi cha wanajeshi wetu ambacho kilikua kinaundwa na wanajeshi kutoka Bangladesh na Pakistan kimeshambuliwa kiliomita 11 na mji wa Bangui na kusababisha kifo cha mwanajeshi wetu mmoja kutoka Pakistan, huku wanajeshi wengine tisa wakijeruhiwa, akiwemo mmoja ambaye hali yake ni mahututi”, amesema mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, Bubacar Gaye.

Hayo yanajiri wakati hali usalama inaendelea kudorora siku baada ya siku mjini Bangui. Jumatano wiki hii watu wawili kutoka jamii ya Waislam waliuawa na watu wanaosadikiwa kuwa wanamgambo wa kikristo wa Anti-balaka. Wanamgambo hao wamekua wakiweka vizuizi kwenye barabara za baadhi ya maeneo ya mji wa Bangui.

Akihojiwa na RFI, Waziri mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Mahamat Kamoun, amelani madai ya Anti-balaka ya kumtaka rais Samba-Panza ajiuzulu.

“ Hatuwezi kuvumilia makundi ambayo hayajulikani kisheria yakiendelea kuwateka raia na kuhatarisha usalama wao. Tunaomba Minisca na kikosi cha wanajeshi wa kimataifa kuyapokonya silaha makundi hayo”, amesema Kamoun.

“ Tumemuomba Waziri wa sheria kuchukua hatua zinazo hitajika ili kuwakamata na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria wahusika wa machafuko hayo”, ameongeza Kamoun.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.