Pata taarifa kuu
CAR-MISCA- AU-UN-Usalama-Siasa

CAR: Misca chini uongozi wa UN

Umoja wa Mataifa unachukuwa rasmi uongozi wa kikosi cha kulinda amani nchini jamhuri ya Afrika ya kati Misca, jukumu lililokuwa chini ya uongozi wa vikosi vya Muungano wa nchi za Afrika ya kati Misca.

Kikosi cha Misca kilitumwa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati tangu Desemba mwaka 2013.
Kikosi cha Misca kilitumwa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati tangu Desemba mwaka 2013. AFP PHOTO / SIA KAMBOU
Matangazo ya kibiashara

Sherehe maalum zimepangwa kufanyika jumatatu wiki hii katika uwanja wa ndege wa jijini Bangui ambapo viongozi wa Misca watakabidhi uongozi kwa kikosi cha Umoja wa Mataifa Minusca kitachoendelea na jukumu la kulinda amani ambacho hadi sasa kinasaidiwa na kikosi cha ufaransa katika operesheni Sangaris na kikosi cha Umoja wa Ulaya nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati Eufor.

Wanajeshi kutoka Pakistan, Bangladesh na Morocco watajiunga na kikosi hicho, kitachofikisha jumla ya askari 7,500 ambao kwa kushirikiana na askari hao wa Afrika watakuwa na kibarua cha kurejesha usalama nchini humo chini ya uongozi wa Jenerali Babacar Gaye.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, amebaini kwamba hatua hiyo inaonyesha kufaulu kwa kikosi cha Umoja wa Afrika kulingana na majukumu kiliyopewa.

“ Kikosi cha Misca kubadili uongozi na kuwa chini ya uongozi wa Umoja wa Mataifa ni kufaulu kwa kikosi hicho kwa majukumu kiliyopewa nchini jamhuri ya Afrika ya Kati”, amesema Ban Ki-moon, huku akitolea wito wahusika katika mgogoro nchini jamhuri ya Afrika ya Kati kusitisha machafuko na kuendeleza siasa kwa lengo la kulijenga taifa hilo.

“ Majukumu yetu ni kulinda raia, na kusaidia mchakato wa kisiasa na kutoa mchango wetu kwa kuweka taasisi za uongozi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati”, amesema mkuu wa Minusca jenerali Babacar Gaye.

Jamhuri ya Afrika ya Kati, imekumbwa na machafuko ya wenyewe kwa wenyewe tangu kutimuliwa madarakani kwa rais François Bozizé na waasi wa Seleka, ambao wengi wao ni kutoka jamii ya Waislam katika taifa lenye wakristo wengi.
Machafuko hayo yamesababisha vifo vya watu wengi na wengine wengi wamekimbilia nje ya nchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.