Pata taarifa kuu
CAR-SELEKA-ANTIBALAKA-Makubaliano-Uteuzi-Siasa

CAR: Catherine Samba-Panza amteua Waziri mkuu mpya

Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Catherine Samba-Panza amemteuwa Mahamat Kamoun kuwa waziri mkuu mpya wa serikali ya mpito kuchukuwa nafasi ya Andre Nzapayeke aliyejiuzulu tarehe 5 Agosti mwaka huu.

rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Catherine Samba-Panza, amemteua Mahamat Kamoun kuwa waziri mkuu mpya.
rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Catherine Samba-Panza, amemteua Mahamat Kamoun kuwa waziri mkuu mpya. REUTERS/Francois Lenoir
Matangazo ya kibiashara

Mahamat Kamoun, ni waziri mkuu wa kwanza muislam aliyetangazwa siku ya jumapili kwenye redio na televisheni ya taifa nchini humo na ambaye hapo awali, alikuwa mkurugenzi wa Ofisi ya rais wa zamani na Kiongozi wa waasi wa Seleka Michel Djotodia, na baadae waziri wa nchi na mshauri maalum wa rais Catherine Samba-Panza.

Katika mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Bangui, makundi ya wanasiasa yamepigwa na bumbu wazi baada ya kuteuliwa kwa Mahamt Kamoun, licha ya kuwa jina lake lilikua limepewa na fasi kubwa ya kuteuliwa kwenye wadhifa huo.

Waziri huyu mkuu mpya hakua miongoni mwa majina yaliyopendekezwa na Ufaransa aidha jumuiya ya kimataifa, ambayo yalikua yamependekeza jina la mtu la Karim Meckassoua.

Jina la Meckassoua lilitupiliwa mbali na waasi wa zamani wa Seleka, wakidai kwamba aliwahi kuhudumu kama waziri katika serikali ya Bozizé.

Uteuzi huo wa Mahamat Kamoun, ambaye hajulikani na taasisi za kimataifa unaonesha wazi kwa namna moja ama nyingine uhuru wa rais Panza kwa kuendesha shughuli zake kama rais kwa ya jumuiya ya kimataifa. Catherine Samba-Panza ameonesha pia uhuru wake kwa waasi wa zamani wa Seleka, ambao hawakukiria kwamba atamteua mtu aliye na ushirikiano wa karibu naye.

Wakati huo huo waasi wa zamani wa Seleka wamebaini kwamba hawatoshiriki katika serikali inayotazamiwa kuundwa hivi karibuni, kwa sababu hawakushirikishwa katika uteuzi wa Mahamat Kamoun. Kutokana na kukabiliwa kwa mgawanyiko, Seleka haikupendekeza jina la mgombea kwa muda uliyotolewa na rais Catherine Samba-Panza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.