Pata taarifa kuu
CAR-SELEKA-ANTIBALAKA-Machafuko-Usalama

CAR: mgogoro wa kisiasa waibuka Bangui

Hali ya taharuki imetanda tangu jana Jumatano jioni mjini Bangui baada ya watu wawili kuuawa, huku shughuli zikisimama kwa siku nzima ya leo Alhamisi kutokana na kuzuka kwa machafuko mapya.

watu wakibeba jeneza la mmoja kati ya Waislam waliouawa katika mtaa wa PK5 unaokaliwa na raia wengi kutoka jamii ya Waislam.
watu wakibeba jeneza la mmoja kati ya Waislam waliouawa katika mtaa wa PK5 unaokaliwa na raia wengi kutoka jamii ya Waislam. REUTERS/Siegfried Modola
Matangazo ya kibiashara

Watu wanaodaiwa kuwa wanamgambo wa kikristo wa Anti-balaka wamemuua mtu mmoja kutoka jamii ya Waislam na mwengine ambaye alikua dereva wa taxi katika mji wa Bangui na kusababisha kuzuka kwa machafuko mapya kati ya waislam na wakristo.

Wanamgambo wa Anti-balaka wamedhibiti mitaa ya baadhi ya maeneo ya mji wa Bangui, huku watu kutoka jamii ya Waislam wakiwa na hofu ya kuuawa na wanamgambo hao.

Mkuu wa tume ya Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, jenerali Babacar Gaye, amelani machafuko hayo, huku akitolea wito wa kusitisha machafuko hayo.
Shughuli zimesimama siku nzima alhamisi wiki hii, baada ya milio mingi ya risase kusikika usiku wa Jumatano kuamkia leo Alhamisi katika mji wa Bangui, huku wanamgambo wa Anti-balaka wakiweka vizuizi kwenye barabara za mji wa Bangui.

Polisi ya tume ya Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, Minusma, imefaulu kuondoa baadhi ya vizuizi viliyokua vimewekwa barabarani. Wakati huo huo wanamgambo wa Anti-balaka wakionekana kwenye barabara zinazoingia na kutoka katika mji wa Bangui, huku raia wakisalia makwao.

Kundi la wanamgambo wa kikristo la Anti-balaka lilimpa rais Catherine Samba-Panza muda wa saa 48 tangu Jumapili awe amesha jiuzulu, huku wakitishia kuendelea kusalia barabarani hadi rais huyo atakapojiuzulu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.