Pata taarifa kuu
UFARANSA-USALAMA-UGAIDI

Watuhumiwa wawili katika shambulio lililozimwa ufaransa wafungwa jela

Watu wawili waliotuhumiwa kupanga shambulio "kubwa" katika kipindi cha uchaguzi wamefunguliwa mashitaka, Jumapili hii Aprili 23 na kufungwa jela, amesema mwendesha mashitaka wa Paris.

Wachunguzi wakagua gari za wahusika wa shambuli katika mtaa wa Champs-Elysées mjini Paris, Alhamisi, Aprili 20.
Wachunguzi wakagua gari za wahusika wa shambuli katika mtaa wa Champs-Elysées mjini Paris, Alhamisi, Aprili 20. REUTERS/Reuters Tv
Matangazo ya kibiashara

Baada ya kukabamwa siku ya Jumanne, Aprili 18, katika mji wa Marseille, Clément Baur na Mahiedine Merabet wamefunguliwa mashitaka ikiwa kwa kosa la kushiriki katika kundi la wahalifu wa kigaidi kwa lengo la kuandaa uhalifu kwa kuhatarisha usalama wa watu, kuwashikilia na usafirishaji wa silaha na mabomu. Silaha na kilo tatu za mabomu aina yaTATP, ambapo sehemu moja ambayo ilikua tayari kwa matumizi, viligunduliwa wakati wa kukamatwa kwao.

Watu hao wawili walikamatwa, siku tano kabla ya duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais, shirika la habari la AFP, wakati huo, liliarifu likinukuu vyanzo vilio karibu na uchunguzi.

Alhamisi Aprili 20, kundi la watu wenye silaha walishambulia gari ndogo la polisi katika mtaa wa Champs Elysées na kumuua polisi mmoja na kuwajeruhi vibaya wengine wawili.

Vikosi vya usalam viliingilia kati na kufaulu kumuua kwa risasi mshambuliaji mmoja.

Usalama umeimarishwa wakati huu uchaguzi ncho hiyo ikiwa katika mchakato wa uchaguzi wa urais.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.