Pata taarifa kuu
Ufaransa

Safari za ndege zaanza tena Orly Paris baada ya shambulizi

Safari za ndege katika uwanja wa ndege wa Orly jijini Paris nchini Ufaransa zimeanza kurejea kama kawaida leo Jumapili siku moja baada ya mtu aliyesababisha tahadhari kubwa ya usalama na vurugu za usafiri wakati alipomshambulia na askari kabla ya kupigwa risasi na kufa.

Uwanja wa ndege wa Orly jijini Paris Ufaransa
Uwanja wa ndege wa Orly jijini Paris Ufaransa REUTERS/Charles Platiau
Matangazo ya kibiashara

Wapelelezi wa Kupambana na ugaidi leo Jumapili wamemwachia baba wa mshambuliaji huyo lakini wanaendelea kumshikilia kaka yake na binamu yake ili kupata taarifa za kumhusu Ziyed Ben Belgacem, mwenye umri wa miaka 39 raia wa Ufaransa.

Watu hao watatu wa familia walijipeleka wenyewe kwa polisi , mwendesha mashtaka wa Paris Francois Molins amewaambia waandishi wa vyombo vya habari mwishoni mwa siku ya Jumamosi.

Ziyed Ben Belgacem, ambaye alipigwa risasi na askari jana Jumamosi katika uwanja wa ndege wa Orly jijini Paris ameelezwa kuwa alikuwa tayari “kufa kwa ajili ya Allah” na aliapa kuua wengine.

Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 39 mzaliwa wa Paris aliua wawakati alipo mshambulia askari, kumkabili na kujaribu kuiba silaha yake , na kukomesha saa kadhaa za vurugu.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.