Pata taarifa kuu

Jeshi la Ukraine lakabiliwa na hali ngumu katika kukabiliana na jeshi la Urusi

Jeshi la Ukraine kwa sasa liko katika hali "ngumu kabisa" kuwakabili wanajeshi wa Urusi ambao wako kwenye mashambulizi mashariki na kusini mwa Ukraine baada ya kuuteka mji wa Avdiivka wikendi hii, Kiev ilikiri kupotea mji huo siku ya Jumatatu.

Mwanajeshi wa Ukraine akipakia makombora kwenye kifaru (tanki), katika eneo la Luhansk, Februari 18, 2024.
Mwanajeshi wa Ukraine akipakia makombora kwenye kifaru (tanki), katika eneo la Luhansk, Februari 18, 2024. REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

 

"Hali ni ngumu sana katika sehemu kadhaa katika uwanja wa vita, ambapo askari wa Urusi wamejizatiti vilivyo katika vita hivi. Wanajaeshi wa Urusi wanapata nafasi ya kusonga mbele katika vita hivi kufuatia kucheleweshwa kwa msaada wa nchi za Magharibi kwa Ukraine, Rais Volodymyr Zelensky alitangaza siku ya Jumatatu, Februari 19, katika ujumbe wake wa kila siku. Aliongeza kuwa nchi yake haina silaha za kivita na inahitaji  vifaa vya kivita vya ulinzi wa angani kama vile silaha za masafa marefu.

Mkuu wa nchi wa Ukraine pia alibaini kwamba kuzuiwa kwa mpaka na Poland na wasafirishaji wa malori na wakulima wa Poland kunaonyesha "kuzorota kwa mshikamano" kwa nchi yake.

Katika uwanja wa vita, askari wa Urusi, ambao wamepata ushindi wao wa kwanza tangu kutekwa kwa Bakhmut mnamo mwezi Mei 2023 kwa kuchukua udhibiti wa Avdiïvka, katika mkoa wa mashariki wa Donetsk, walifanya shambulio mashariki na kusini, limeelezea jeshi la Ukraine.

Katika sehemu ya kusini ya uwanja wa vita, "adui amefanya majaribio kumi bila kufanikiwa dhidi ya ngome za vikosi vya ulinzi vya (Ukraine) katika eneo (la kijiji) cha Robotyne. Hapa, hali inabadilika, adui anatoa moto mkali,” amesema Dmytro Lykhovy, msemaji wa jeshi la Ukraine katika eneo hili.

Mashambulizi mengi ya Urusi

Kulingana na yeye, Waukraine walizuia mashambulio yaliyoanzishwa "na idadi kubwa ya magari ya kivita" lakini Warusi sasa wanashambulia na "makundi madogo"yanayosaidiwa na magari ya kivita na jeshi la anga ambalo "linafanya kazi kikamilifu".

"Majaribio haya ya yamesitishwa, adui ameondolewa nje kidogo ya Robotyne," amesema Jenerali Oleksandr Tarnavsky, kamanda wa askari wa Ukraine katika eneo hilo. Kituo cha Telegram cha DeepState, kilicho karibu na jeshi la Ukraine, kiliripoti siku ya Jumapili jioni kwamba wanajeshi wa Urusi walifanikiwa kupenya ngome ya Ukraine kilomita chache mashariki mwa Robotyne.

Kijiji hiki, kama maeneo mengine mengi ambayo yaliteketezwa kabisa na mizinga, kilichukuliwa tena kutoka kwa Warusi mnamo mwezi wa Agosti, ambapo ilielezewa kama mafanikio muhimu na Ukraine katika mashambulio ambayo ilikuwa imeanzisha msimu wa joto.

Mashambulizi ya Urusi katika sehemu hii ya vita ya kusini yalianza wikendi hii wakati jeshi la Urusi lilipoteka Avdiïvka, takriban kilomita 150 kaskazini mashariki mwa Robotyne, baada ya miezi minne ya mashambulio ya mara kwa mara.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.