Pata taarifa kuu

Ukraine yaupoteza mji wa viwanda wa Avdiïvka, Urusi yafurahia ushindi

Baada ya mapigano ya miezi kadhaa, hatimaye jeshi la Ukraine limeondoka katika mji wa Avdiivka ulioko mashariki mwa nchi hiyo. "Uamuzi wa haki" kwa "kuokoa maisha ya watu wengi iwezekanavyo," amesema Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky Jumamosi Februari 17 kutoka kwenye jukwaa la Mkutano wa Usalama wa Munich. Je, ni matokeo gani kwa Ukraine na kwa Urusi katika vita hivi vinavyodumu kwa miaka miwili sasa? 

Avdiïvka, Februari 15, 2024.
Avdiïvka, Februari 15, 2024. REUTERS - RFE/RL/SERHII NUZHNENKO
Matangazo ya kibiashara

 

Vikosi vya Ukraine vimeondoka katika mji wa kimkakati wa mashariki wa Avdiivka, ambapo hali imetajwa kuwa tete katika siku za hivi karibuni.

Kiongozi wa kijeshi kwenye mji wa viwanda wa Avdiivka, Jenerali Oleksandr Tarnavsky amesema uamuzi wa kuwaondoa wanajeshi umefanyika ili kuzuia mzingiro kutoka kwa viosi vya Urusi, pamoja na kulinda afya wapiganaji hao.

Ikiwa habari hii itathibitishwa itakuwa pigo kubwa kwa serikali mjini Kyiv ambayo askari wake wamekuwa wakipambana kuikabili Urusi tangu vita vilipozuka mwezi Februari 2022.

Awali maafisa wa kijeshi wa Ukraine na Marekani walisema kuna uwezekano mkubwa kuwa vikosi vya Urusi vinaweza kuukamata mji huo hivi karibuni.

Mji wa Avdiivka uliopo katika mkoa wa Donetsk nchini Ukraine umeshuhudia mapigano makali  kwa takriban miaka miwili ya uvamizi wa Urusi. Moscow inadai mji huo ni sehemu ya milki yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.