Pata taarifa kuu

Ukraine: Sasa si wakati wa kufanya uchaguzi, anasema Volodymyr Zelensky

Uchaguzi wa wabunge na urais ulipaswa kufanyika msimu huu wa masika na msimu ujao wa mvua. Sasa sio wakati, anasema Volodymyr Zelensky. Rais wa Ukraine anahalalisha uamuzi wake kwa kutumia sababu rahisi sana: vita dhidi ya Urusi ambayo inafanya utendaji wa kawaida wa demokrasia ya Ukraine kutowezekana machoni pake.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akiwatuza wanajeshi karibu na Bakhmut, mashariki mwa Ukraine, Julai 29, 2023.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akiwatuza wanajeshi karibu na Bakhmut, mashariki mwa Ukraine, Julai 29, 2023. © Ukrainian Presidential Press Service via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Ni mjadala ambao umechochea wanasiasa wa Ukraine kwa miezi kadhaa: ikiwa chaguzi hizi zingepangwa - uchaguzi wa wabunge ungefanyika Oktoba mwaka huu na uchaguzi wa urais mnamo Machi 2024 - katika muktadha wa vita, na 20% ya eneo linalokaliwa, matatizo ya usalama yanayotokana na milipuko ya mabomu ya Urusi, na kwa kukosekana kwa mamilioni ya Waukraine waliokimbia nchi. Katika muktadha wa usalama usio wa kawaida kabisa na nchi iliyohamasishwa kabisa katika juhudi za vita na chini ya sheria za kijeshi.

Volodymyr Zelensky hatimaye ametatua mjadala huu, na alitangaza jana katika hotuba yake ya kila siku. "Lazima tuamue kwamba huu ni wakati wa ulinzi, kwa vita, ambayo hatima ya serikali na watu inategemea, na sio mchezo wa kuchekesha, ambao Urusi pekee inatarajia kutoka Ukraine. Nadhani sasa si wakati wa uchaguzi. "

Hoja nyingine iliyotolewa na rais wa Ukraine: chaguzi hizi hazingewezekana tu kuandaa, lakini pia zingeweza kuhatarisha kuongeza mgawanyiko ndani ya jamii ya Waukrane. Na hii katika wakati ambapo mashaka yanaongezeka juu ya mwenendo wa vita, na kushindwa kwa mashambulizi ya kukabiliana, na hofu ya kuona uungwaji mkono wa washirika wake wa Magharibi ukiishiwa na nguvu. Kwa mtazamo huu, uamuzi wa Rais Zelensky ni nyeti, kwa sababu Marekani, mshirika mkuu wa Kiev, ilitaka uchaguzi huu ufanyike, na ufanyike licha ya vita.

Tangazo la Volodymyr Zelensky linakuja huku Urusi ikiendelea kufanya mashambulizi makali kila siku katika takriban maeneo yote ya Ukraine. Kiev iliishutumu tena Moscow jana, Jumatatu, kwa kurusha makombora manne usiku na kurusha ndege zisizo na rubani kutoka maeneo ya Ukraine yanayokaliwa na Urusi kusini mwa nchi hiyo. Na Wizara ya Ulinzi ya Urusi imetangaza kwa upande wake kwamba ulinzi wa anga wa Urusi uliharibu na kunasa ndege zisizo na rubani 17 zilizorushwa na Ukraine usiku wa Jumatatu kuamkia Jumanne juu ya Bahari Nyeusi na rasi ya Crimea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.