Pata taarifa kuu

Vita nchini Ukraine: Urusi yasema imechukua udhibiti wa Marïnka mashariki mwa Ukraine

Jeshi la Urusi limeudhibiti mji wa Marïnka, karibu na Donetsk mashariki mwa Ukraine, Waziri wa Ulinzi wa Urusi Sergei Shoigu alisema siku ya Jumatatu. Madai hayo, hata hivyo, yamekanushwa na jeshi la Ukraine siku ya Jumanee. Msemaji, Oleksandr Chtoupoun, amesema "sio sahihi" kusema mji huo unadhibitiwa kabisa na Urusi.

Wanajeshi wa jeshi la Ukraine wanatembea kando ya barabara katika mji wa Marïnka katika Mkoa wa Donetsk, Ukraine Aprili 14, 2021.
Wanajeshi wa jeshi la Ukraine wanatembea kando ya barabara katika mji wa Marïnka katika Mkoa wa Donetsk, Ukraine Aprili 14, 2021. REUTERS - ANASTASIA VLASOVA
Matangazo ya kibiashara

"Mapigano ya Marïnka yanaendelea," amesema, na kuongeza kuwa bado kuna askari wa Ukraine katika mji huo, ambao "umeharibiwa kabisa." "Mji wa Marinka, ulioko kilomita tano kusini magharibi mwa Donetsk, umekombolewa kabisa leo," Sergei Shoigu alitangaza hapo awali wakati wa mahojiano ya televisheni na Rais Vladimir Putin.

Marïnka ilibadilishwa na jeshi la Ukraine kuwa ngome tangu mwaka 2014 na kuanza kwa mzozo na watu wanaotaka kujitenga wanaounga mkono Urusi wakiongozwa na Moscow, ambao waliuteka mji wa Donetsk. Kulingana na Sergei Shoigu, Marïnka ni “eneo lenye ngome lenye nguvu lililounganishwa na njia za chini ya ardhi” ambazo huilinda dhidi ya mizinga na mashambulizi ya anga. "Kutokana na hatua zenye maamuzi za askari wetu, ngome ilipasuka," alisema.

Vladimir Putin akaribisha kutekwa kwa Marïnka

"Ukombozi wa eneo hilo kwa kawaida hupunguza uwezo wa ulinzi wa Kikosi cha Wanajeshi wa Ukraine na hutupatia fursa zaidi za kuendelea na hatua yetu katika mwelekeo huu," aliongeza.

Vladimir Putin amekaribisha ukweli kwamba kutekwa kwa Marïnka kunawaweka wanajeshi wa Ukraine mbali na Donetsk, mji mkuu wa eneo hilo chini ya udhibiti wa Urusi ambao umekuwa ukilengwa mara kwa mara na milipuko ya mabomu ya Ukraine tangu mwaka 2014. "Tumerudisha nyuma kikosi cha mizinga cha Ukraine karibu na Donetsk [... ] na hii leo inafanya uwezekano wa kulinda Donetsk kwa ufanisi zaidi dhidi ya mashambulizi,” pia alisisitiza Sergei Shoigu.

Marïnka, kama eneo la kimkakati, "inawapa wanajeshi wetu uwezekano wa kuwa na nafasi pana ya kufanya kazi", kwa upande wake amethibitisha Vladimir Putin. Vikosi vya Urusi vimerejesha mpango huo wa mbele tangu kushindwa kwa mashambulio ya Ukraine, na kupata mafanikio hasa Mashariki. Hasa, wamekuwa wakijaribu kwa miezi kadhaa kuzunguka ngome nyingine, ile ya Avdiïvka, pia Mashariki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.