Pata taarifa kuu

Mshirika wa zamani wa Prigozhin kuongoza wapiganaji wa kujitolea Ukraine

Nairobi – Andrei Troshev, kamanda za zamani wa mamluki wa Wagner, amepewa jukumu la kuvisimamia vikosi vya wapiganaji wakujitolea nchini Ukraine, baada yake kukutana na rais Vladimir Putin ambaye alimpa majukumu hayo.

Uteuzi wake katika wadhifa huo umeafikiwa baada ya kikao kati yake ya rais Vladimir Putin
Uteuzi wake katika wadhifa huo umeafikiwa baada ya kikao kati yake ya rais Vladimir Putin via REUTERS - SPUTNIK
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa taarifa ya msemaji wa Kremlin, Dmitry Peskov , kiongozi huyo wa zamani wa Wagner kwa sasa ni mfanyikazi wa wizara ya ulinzi ya Urusi.

Uteuzi wake katika wadhifa huo umeafikiwa baada ya kikao kati yake ya rais Vladimir Putin, kilichojadili nafasi ya wapiganaji wa kujitolea katika mzozo wa Ukraine.

Rais Putin amempa afisa huyo wa zamani wa Wagner majukumu hayo
Rais Putin amempa afisa huyo wa zamani wa Wagner majukumu hayo AFP - MIKHAIL METZEL

Wachambuzi wa masuala ya kimataifa wanasema hatua hii ya kremlin huenda inatuma ujumbe kwa dunia kuwa Urusi kwa sasa imechukua uthibiti wa Wagner baada ya jaribio  la uasi dhidi ya utawala wa Putin mwezi Juni kutofanikiwa.

Yevgeny Prigozhin alidaiwa kufariki katika ajali ya ndege
Yevgeny Prigozhin alidaiwa kufariki katika ajali ya ndege REUTERS - STRINGER

Msikilizaji ikumbukwe kuwa uasi huo wa muda mfupi uliongozwa na mkuu wa Wagner Yevgeny Prigozhin, ambaye baadae mwezi Agosti alidaiwa kufariki katika ajali ya ndege.

Kwa mujibu wa taarifa ya msemaji wa Kremlin, Dmitry Peskov , kiongozi huyo wa zamani wa Wagner kwa sasa ni mfanyikazi wa wizara ya ulinzi ya Urus
Kwa mujibu wa taarifa ya msemaji wa Kremlin, Dmitry Peskov , kiongozi huyo wa zamani wa Wagner kwa sasa ni mfanyikazi wa wizara ya ulinzi ya Urus via REUTERS - SPUTNIK

Troshev alihusika pakubwa katika oparesheni za Wagner wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria kwa mujibu wa stakabadhi za Umoja wa Ulaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.