Pata taarifa kuu

Vita nchini Ukraine: Meya wa Kyiv asema Zelensky 'analipa kwa makosa aliyofanya'

Meya wa Kiev Vitali Klitschko anaamini kwamba Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky "analipa makosa aliyofanya" na kwamba raia wa Ukraine wanapoteza imani na kiongozi wao katika vita anayoendesha dhidi ya Urusi, vyombo vya habari kadhaa vya kigeni vinaripoti.

Katika mahojiano ya awali na Gazeti la Der Spiegel, meya wa Kyiv alielezea aina ya ubabe kwa Volodymyr Zelensky na kuzingatia kwamba "wakati fulani, hatutakuwa tofauti sana na Urusi, ambapo kila kitu kinategemea utashi wa 'mtu mmoja'.
Katika mahojiano ya awali na Gazeti la Der Spiegel, meya wa Kyiv alielezea aina ya ubabe kwa Volodymyr Zelensky na kuzingatia kwamba "wakati fulani, hatutakuwa tofauti sana na Urusi, ambapo kila kitu kinategemea utashi wa 'mtu mmoja'. AP - Efrem Lukatsky
Matangazo ya kibiashara

Vitali Klitschko, wakati bado anasema anamuunga mkono rais wake, anaamini kwamba mwisho wa vita kati ya Ukraine na Urusi, "kila mwanasiasa atalipia mafanikio yake au kushindwa kwake."

"Watu wanaona ni nani anayefaa na nani asiyefaa. Kulikuwa na bado kuna matarajio mengi. Zelensky analipa makosa aliyofanya," kiongozi huyo ameambia vyombo vya habari vya Uswizi vikinukuliwa na Sky News.

"Watu wanashangaa kwa nini hatukuwa tumejitayarisha vyema kwa vita hivi, kwa nini Zelensky alikanusha hadi mwisho kwamba vita havitachukuwa muda mrefu," Vitali Klitschko ameongeza.

"Lazima tumuunge mkono hadi mwisho wa vita"

Meya wa Kyiv pia anasema anashangaa kuhusu siku za kwanza za mzozo wakati wanajeshi wa Urusi waliingia katika eneo la Ukraine na kufika "haraka" kuelekea mji mkuu.

"Rais bado ana kazi muhimu leo ​​na lazima tumuunge mkono hadi mwisho wa vita", anarekebisha kidogo Vitali Klitschko, "mwisho wa vita hivi, kila mwanasiasa atalipa mafanikio yake au kushindwa kwake."

Katika mahojiano ya awali na Gazeti la Der Spiegel, meya wa Kyiv alielezea aina ya ubabe kwa Volodymyr Zelensky na kuzingatia kwamba "wakati fulani, hatutakuwa tofauti sana na Urusi, ambapo kila kitu kinategemea utashi wa 'mtu mmoja'.

Vita kati ya Kyiv na Moscow vilichukua mkondo wa kuongezeka kwa operesheni za kijeshi za Urusi mashariki mwa Ukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.