Pata taarifa kuu

Uingereza kuendelea kusimama na Ukraine: David Cameron

Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza David Cameron ambaye amefanya ziara jijini Kyiv na kukutana na rais Volodymyr Zelensky, ameahidi kuendeleza msaada wa kijeshi kwa Ukraine.

Uingereza imekuwa mshirika wa karibu wa Ukraine tangu uvamizi wa urusi
Uingereza imekuwa mshirika wa karibu wa Ukraine tangu uvamizi wa urusi via REUTERS - UKRAINIAN PRESIDENTIAL PRESS SER
Matangazo ya kibiashara

Waziri mkuu huyo wa zamani amefanya ziara yake ya kwanza jijini Kyiv tangu ateuliwe kuhudumu katika wadhifa wa waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza.

London imekuwa mshirika wa karibu wa Ukraine tangu uvamizi wa Moscow ambapo pia imeendelea kuungana na mataifa mengine washirika wa Kyiv kutoa msaada wa kijesi nchini Ukraine.

Kwa mujibu wa Cameron, nchi yake itandelea kutoa msaada kwa Ukraine ikiwemo uungwaji mkono katika masuala ya kidiplomasia, kiuchumi na kijeshi mwaka huu na mwaka ujao.

Kwa upande wake rais  Zelensky amemshukuru Cameron kwa kuikumbuka nchi yake wakati huu dunia nzima ikielekeza macho yake kuhusu kinachoendelea katika Mashariki ya kati.

Viongozi hao wamejadiliana kuhusu masuala mbalimbali likiwemo suala la utengenezaji wa silaha
Viongozi hao wamejadiliana kuhusu masuala mbalimbali likiwemo suala la utengenezaji wa silaha via REUTERS - UKRAINIAN PRESIDENTIAL PRESS SER

Wizara ya nje ya Ukraine imesema waziri Cameron amefanya mazungumzo kuhusu masuala ya utengenezaji wa silaha na ulinzi katika bahari nyeusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.