Pata taarifa kuu

Ukraine yakusanya euro bilioni 60 kwa ajili ya ujenzi wake

Ukraine na washirika wake wanajaribu kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa nchi hiyo. Mkutano katika mwelekeo huu ulifanyika tangu Jumatano hii huko London na hadi siku ya Alhamisi jioni euro bilioni 60 zingine zimetolewa.

Mkutano wa ujenzi mpya wa Ukraine huko London, Juni 22.
Mkutano wa ujenzi mpya wa Ukraine huko London, Juni 22. AP - Kirsty Wigglesworth
Matangazo ya kibiashara

Ikiwa vita vitasimama leo, kurejesha uchumi wa Ukraine na kujenga upya nchi kutagharimu zaidi ya dola bilioni 400, Benki ya Dunia inakadiria. Hii ni mara mbili ya Pato la Taifa la Ukraine kabla ya vita. Kwa hivyo Kyiv inawaalika washirika wake na makampuni ya kibinafsi kusaidia kujenga upya nchi hiyo sasa. Waziri Mkuu wa Ukraine, Denys Chmyhal, amesisitiza hili mwishoni mwa mkutano huo, ambapo alishiriki.

"Ujenzi mpya wa Ukraine utafaidi sio tu Ukraine, lakini pia washirika wetu na wafadhili. Huu pia utakuwa mchango muhimu kwa uchumi wa Ulaya. Hii inawakilisha fursa na matarajio ya ziada kwa biashara kote ulimwenguni. Ujenzi mpya wa Ukraine ni mradi mkubwa zaidi barani Ulaya tangu Vita vya Pili vya Dunia,” amesema Waziri Mkuu wa Ukraine.

Bilioni 50 zilizoahidiwa na Umoja wa Ulaya

Umoja wa Ulaya uliahidi euro bilioni 50 saa chache kabla ya kufunguliwa kwa mkutano huo. Bilioni 10 zaidi zilitangazwa wakati wa hafla hiyo, hasa kutoka Uingereza, Marekani na hata Benki ya Dunia.

Sehemu ndogo itatolewa kwa haraka, iliyobaki kwa muda wa kati na mrefu. Mamlaka ya Uingereza pia inahakikisha kwamba makampuni 500 ya kibinafsi, kutoka karibu nchi arobaini tofauti, yameahidi kuwekeza ili kujenga upya nchi hiyo. Lakini hawakutaja kwa kiasi gani.

Mkuu wa serikali ya Ukraine pia amekaribisha ahadi ya "karibu washiriki wote" kuunga mkono wazo kwamba Urusi italazimika "kulipa uhalifu wake na uharibifu iliyosababisha nchini Ukraine". "Lazima tukamilishe utaratibu wa fidia ambao utaturuhusu kutumia mali ya Urusi iliyozuiwa kuijenga upya Ukraine," amebaini, wakati mijadala ya kimataifa bado inakwama kuhusu mipango ya kisheria.

Madhumuni ya mkutano huu wa London ilikuwa ni kukusanya fedha muhimu kwa ajili ya ujenzi wa Ukraine katika muda mfupi na wa kati, lakini pia kutoa wito kwa sekta binafsi kuchangia, kwa kuweka utaratibu wa kuhakikisha uwekezaji wao nchini humo, wakati jeshi. bado liko katika vita kamili dhidi ya vikosi vya Urusi.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.