Pata taarifa kuu

Wanajeshi 30,000 wa Ukraine watafunzwa na nchi za EU mnamo 2023

Nchi za Umoja wa Ulaya zitatoa mafunzo kwa wanajeshi 30,000 wa Ukraine mwaka huu, Wizara ya Ulinzi ya Ukraine imetangaza leo Jumanne, huku jeshi lake likizindua jaribio la kukabiliana na mashambulizi yanayolenga kukomboa maeneo yanayokaliwa na Urusi. 

Wanajeshi wa Ukraine wakiwa katika operesheni karibu na Kreminna, katika eneo la Luhansk, Juni 8.
Wanajeshi wa Ukraine wakiwa katika operesheni karibu na Kreminna, katika eneo la Luhansk, Juni 8. © ROMAN CHOP/AP/SIPA
Matangazo ya kibiashara

"Mnamo mwaka 2023, ndani ya mfumo wa ujumbe wa usaidizi wa kijeshi wa Umoja wa Ulaya nchini Ukraine, imepangwa kutoa mafunzo kwa wanajeshi 30,000 wa vikosi vya wanajeshi wa Ukraine, wakiwemo askari wa vikosi vya ulinzi w aUkraine," wizara hiyo imesema.

Kundi la nchi Ishirini na Saba wanachama wa Umoja wa Ulaya, lilianzisha programu mnamo mwezi Novemba inayolenga kutoa mafunzo kwa wanajeshi wa Ukraine 15,000 katika nchi zake mbalimbali wanachama.

"Idadi hii labda itafikiwa kabla ya mwisho wa robo ya pili ya mwaka huu na kutakuwa na lengo jipya la mafunzo ya wanajeshi 15,000 wa Ukraine na nchi tofauti za Ulaya," afisa moja wa Ulaya alisema, kwa sharti la kutotajwa jina.

Mafunzo hayo yanafanyika katika nchi kadhaa za Ulaya, ambapo kituo kikuu cha misheni hiyo kiko Poland, nchi inayopakana na Ukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.