Pata taarifa kuu

Ukraine: Macron kuionya Beijing dhidi 'uamuzi wowote mbaya' wa kuunga mkono Moscow kijeshi

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron atamuonya mwenzake wa China Xi Jinping wiki ijayo nchini China kuhusu matokeo ya uwezekano wa 'uamuzi mbaya' wa kuunga mkono Urusi kijeshi dhidi ya Ukraine, Ikulu ya Elysee imesema siku ya Ijumaa

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akizungumza wakati wa mahojiano ya televisheni kutoka Ikulu ya Elysée huko Paris.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akizungumza wakati wa mahojiano ya televisheni kutoka Ikulu ya Elysée huko Paris. AFP - LUDOVIC MARIN
Matangazo ya kibiashara

"Ikiwa China itachukua uamuzi huu mbaya, kuna athari kubwa ya kimkakati kwenye mzozo," mshauri wa rais wa Ufaransa amesema. Amebainisha kuwa Rais Macron ametaka "kutafuta nafasi" na Beijing kwa "mipango" ili "kuunga mkono raia wa Ukraine", lakini pia "kutambua njia ya muda wa kati kwa suluhisho la mzozo".

"Tunataka kuepuka mabaya na ndiyo maana inatubidi kuwashawishi, ili kuwaonyesha msimamo wetu kwao," ameongeza mbele ya waandishi wa habari wachache. Kwa mujibu wa ofisi ya rais wa Ufaransa, mazungumzo haya ni muhimu zaidi kwani "China ndiyo nchi pekee duniani yenye uwezo wa kuwa na athari za haraka na kali kwenye mzozo huo, katika mwelekeo mmoja au mwingine".

Emmanuel Macron anaenda China kuanzuia Jumatano hadi Ijumaa kwa ziara ya serikali inayolenga kuweka katika vitendo "mbinu hii" baada ya muda mrefu bila mawasiliano ya wawili hao kwa sababu ya mlipuko wa UVIKO-19, yaliyovunjwa na mkutano na Xi Jinping mnamo mwezi Novemba kando ya mkutano wa kilele nchini Indonesia.

Paris inahukumu Beijing katika changamoto nyingi za kimataifa, kwanza kabisa mapambano dhidi ya ongezeko la joto duniani. Kuhusu mzozo wa Ukraine, China, ambayo haijawahi kulaani uvamizi wa Urusi, ni "game changer", amesema mshauri huyo, akitumia usemi wa Kiingereza kuelezea kuwa mtazamo wake unaweza kuathiri mkondo wa vita.

Ufaransa ilitarajia hadi hivi majuzi kumshawishi rais wa China kutumia "ushawishi" wake kwa mwenzake wa Urusi Vladimir Putin ili kumsukuma kuelekea mazungumzo kuhusu mzozo. Hata kwamba ina "jukumu la upatanishi".

Lakini ziara ya Xi Jinping huko Moscow siku kumi zilizopita, ambapo viongozi hao wawili walisifu uhusiano wao "maalum" na kushambulia vikali nchi za Magharibi, inaonekana kuwa imesababisha mamlaka ya Ufaransa kupunguza matarajio yake. "Tuna akili timamu," amesema rais wa Ufaransa, akibainisha hasa kwamba China haina nia ya kulaani Urusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.