Pata taarifa kuu

Putin na XI waidhinisha mradi wa bomba kubwa la gesi kati ya Urusi na China

Rais wa Urusi Vladimir Putin na mwenzake wa China Xi Jinping wamefikia makubaliano juu ya mradi mkubwa wa gesi wa Siberia 2 siku ya Jumanne, ishara ya nia ya Moscow ya kuelekeza uchumi wake kuelekea Asia dhidi ya vikwazo vya kimataifa.

Xi Jinping na Vladimir Putin wakualiana kuanzisha ushirikiano katika mradi mkubwa wa bomba la gesi.
Xi Jinping na Vladimir Putin wakualiana kuanzisha ushirikiano katika mradi mkubwa wa bomba la gesi. AFP - GRIGORY SYSOYEV
Matangazo ya kibiashara

"Makubaliano yote yamehitimishwa" kwa utekelezaji wa mradi mkubwa wa bomba la gesi wa Siberia 2, baada ya majadiliano kati ya wajumbe wa Urusi na China. "Mradi huu ukitekelezwa," alisema, "mita za ujazo bilioni 50 za gesi" zitapitia bomba hili la kilomita 2,600 ambalo litaunganisha Siberia na jimbo la Xinjiang Kaskazini Magharibi mwa China, kupitia Mongolia.

Tangazo hili litaezesha Urusi kuongeza kwa kiasi kikubwa usafirishaji wake wa gesi kwenda China, wakati uchumi wake utabadili mwelekeo katika soko la Ulaya tangu vikwazo vilivyofuatia uvamizi nchini Ukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.