Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Xi Jinping katika ziara ya serikali ya 'amani' nchini Urusi

Marais wa China na Urui Xi Jinping na Vladimir Putin Jumatatu wamekaribisha nguvu ya ushirikiano wao wa pande mbili, saa chache kabla ya rais wa China kuwasili Moscow kwa mkutano wa kilele na mwenzake wa Urusi aliyetengwa kimataifa.

Rais wa Urusi Vladimir Putin na Rais wa China Xi Jinping Februari 4, 2022 mjini Beijing.
Rais wa Urusi Vladimir Putin na Rais wa China Xi Jinping Februari 4, 2022 mjini Beijing. © ALEXEI DRUZHININ / AP
Matangazo ya kibiashara

Ziara hiyo ya kiserikali ya siku tatu nchini Urusi, nchi ambayo China ina uhusiano muhimu wa kidiplomasia na kiuchumi, ni ya kwanza kwa kiongozi huyo wa China kwa jirani yake katika kipindi cha karibu miaka minne.

Katika makala iliyochapishwa katika gazeti la Urusi la Rossiyskaya Gazeta, Xi Jinping ametangaza ziara yake kama "ziara ya urafiki, ushirikiano na amani", dhidi ya nchi za Magharibi zinazotilia shaka uhusiano wa China na Urusi.

"Ninatarajia kufanya kazi na Rais Putin kwa pamoja kupitisha maono mapya" ya uhusiano wa nchi mbili, ameandika Bw. Xi .

Kwa nguvu ya kuwezesha maridhiano ya hivi karibuni ya kidiplomasia kati ya Saudi Arabia na Iran, China inajiweka kama mpatanishi wa vita vya Urusi na Ukraine na kutoa wito hasa wa mazungumzo ya amani kati ya Moscow na Kiev.

Katika makala iliyochapishwa Jumatatu katika gazeti la China, Vladimir Putin anapongeza "utayari wa China kuchukua jukumu la kujenga katika utatuzi" wa mzozo huo na anaamini kwamba "uhusiano wa Urusi na China umefikia hatua ya juu zaidi katika historia yao".

Ziara ya Xi Jinping inakuja siku chache baada ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kutangaza kwamba imetoa hati ya kukamatwa kwa rais wa Urusi, anayetuhumiwa kwa uhalifu wa kivita kwa "kuwachukuwa kinyume cha sheria" watoto wa Ukraine.

 Xi Jinping, ambaye ndio kwanza ameanza muhula wa tatu kama rais, jambo ambalo halijawahi kushuhudiwa nchini China, mara kwa mara humwita Vladimir Putin "rafiki yake wa zamani".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.