Pata taarifa kuu

Mkutano wa kilele wa SCO: Putin na Xi waonyesha mshikamano dhidi ya nchi za Magharibi

Rais Xi Jinping wa China na Rais wa Urusi Vladimir Putin siku ya Alhamisi wameonyesha nia yao ya kusaidiana na kuimarisha uhusiano wao katikati ya mgogoro na nchi za Magharibi, wakati wa mkutano wao wa kwanza tangu kuanza kwa uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Xi Jinping na Vladimir Putin huko Samarkand Julai 15, 2022 wakati wa mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO).
Xi Jinping na Vladimir Putin huko Samarkand Julai 15, 2022 wakati wa mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO). AP - Alexandr Demyanchuk
Matangazo ya kibiashara

Vladimir Putin na Xi Jinping wamekutana kando ya mkutano wa wakuu wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) huko Samarkand, Uzbekistan, wakati uhusiano kati ya nchi zao na Marekani ukiwa na matatizo makubwa. Katika muktadha huu, maelewano kati ya Beijing na Moscow, ambapo mahusiano yao hayako sawa kutokana na mvutano, yanajitokeza dhidi ya Marekani ambayo wanaiona kuwa ni adui dhidi ya maslahi yao.

"China iko tayari kufanya kazi na Urusi katika kuhakikisha majukumu yao kama nchi zenye nguvu, kuchukua nafasi ya kwanza, kwa kuleta utulivu na kuingiza nishati chanya katika ulimwengu wenye machafuko," Xi Jinping amesema mwanzoni mwa mazungumzo yalirushwa moja kwa moja.

Kwa mujibu wa televisheni ya serikali ya China, Xi Jinping pia amemwambia Vladimir Putin kwamba China iko tayari "kufanya kazi na Urusi kwa uungaji mkono thabiti na wa pande zote katika masuala yanayohusiana na maslahi ya msingi ya kila mmoja na kuimarisha ushirikiano". Putin, kwa upande wake, alishutumu majaribio ya nchi za Magharibi ya "kutaka kujikokotea kila kitu na kuchukuwa uamuzi peke yao", ambapo "hivi karibuni hali hiyo ilichukua sura mbaya kabisa na haikubaliki kabisa".

Beijing yaunga mkono Moscow bila kuchukua msimamo kuhusu Ukraine

Mkutano wao wa awali ulifanyika mwezi wa Februari mwaka huu, wakati rais wa Urusi alipohudhuria Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi huko Beijing. Wakati huo walitangaza urafiki wao "bila kikomo". Ikiwa alisifu "msimamo wa usawa" wa Xi Jinping juu ya Ukraine siku ya Alhamisi, rais wa Urusi pia alisema "kuelewa maswali (yake) na wasiwasi (wake) juu ya suala hili. "Tutaelezea msimamo wetu kwa undani," aliongeza, bila maelezo zaidi.

Beijing haijaunga mkono wala kukosoa hadharani uvamizi wa Urusi, huku ikieleza mara kwa mara uungaji mkono wake kwa Moscow katika kukabiliana na vikwazo vya Magharibi.

Kwa mujibu wa televisheni ya serikali ya China, Xi Jinping pia alifanya mazungumzo huko Samarkand na Rais wa Belarus Alexander Lukashenko, mshirika mkuu wa Urusi.

Kana kwamba ni kuashiria kukaribiana kwao katika hali ya mvutano na nchi za Magharibi, meli za Urusi na China zimefanya doria ya pamoja katika Bahari ya Pasifiki siku ya Alhamisi "kuimarisha ushirikiano wao wa baharini", Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema. Vladimir Putin pia amesisitiza uungaji mkono wa Moscow kwa Beijing kuhusu suala la Taiwan, ambapo ziara za maafisa wa Marekani katika wiki za hivi karibuni ziliamsha hasira ya China, na kulaani "uchokozi" kutoka kwa Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.