Pata taarifa kuu

EU yaionya China dhidi ya kuisaidia silaha nchi ya Urusi

NAIROBI – Mkuu wa sera za kigeni wa umoja wa Ulaya, Josep Borrell, ameionya China kuisaidia silaha nchi ya Urusi inayopigana nchini Ukraine, kauli anayotoa saa chache baada ya Beijing kukanusha madai ya Marekani kwamba inafikiria kutuma silaha.

Josep Borrell, Mkuu wa sera za kigeni wa umoja wa Ulaya
Josep Borrell, Mkuu wa sera za kigeni wa umoja wa Ulaya AP - John Thys
Matangazo ya kibiashara

Borrell amesema kwamba amemwambia mwanadiplomasia wa China Wang Yi kuwa hatua hiyo itatafsiriwa kama kuvuka mstari mwekundu katika uhusiano wao, Yi hata hivyo akimhakikishia kuwa hawatafanya hivyo na wala hawana mpango wa kutuma silaha hizo ila watasalia macho.

Siku ya jumapili, waziri wa mambo ya nje wa marekani Antony Blinken, alisema kuwa China ilikuwa inafikiria juu ya kutoa msaada wa silaha mbaya kwa Moscow, lakini China ikatupilia mbali madai hayo na kuyataja kuwa ya uongo, na kusema kuwa Marekani imekuwa ikichochea mzozo kwa kutuma silaha nchini Ukraine.

Kumekuwa na wasiwasi mkubwa juu ya uhusiano wa kina wa Beijing na Moscow na kukataa kwake kulaani uchokozi wa Kremlin moja kwa moja, waziri wa mambo ya nje wa Sweden akionya kuwa iwapo China itaanza kutuma silaha nchini Urusi basi hatua hiyo itakuwa na athari zake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.