Pata taarifa kuu
USALAMA-AJALi

Ugiriki: Safari za treni zaanza tena wiki tatu baada ya ajali mbaya

Baada ya wiki tatu kusitishwa kufuatia jali mbaya ya Februari 28 ambayo iliua watu 57, safari za treni zimeanza tena kwenye katika baadhi ya maeneo ya miji.

Maafisa wa kikosi cha Zima moto na waokoaji wakiendesha shughuli zao baada ya treni mbili kugongaa huko Tempe karibu na jiji la Larissa, Ugiriki, Jumatano, Machi 1, 2023. Treni iliyokuwa imebeba mamia ya abiria iligongana na treni ya mizigo iliyokuwa ikitokeakaskazini mwa Ugiriki, na kuua na kujeruhi makumi ya abiria.
Maafisa wa kikosi cha Zima moto na waokoaji wakiendesha shughuli zao baada ya treni mbili kugongaa huko Tempe karibu na jiji la Larissa, Ugiriki, Jumatano, Machi 1, 2023. Treni iliyokuwa imebeba mamia ya abiria iligongana na treni ya mizigo iliyokuwa ikitokeakaskazini mwa Ugiriki, na kuua na kujeruhi makumi ya abiria. AP - Vaggelis Kousioras
Matangazo ya kibiashara

Wiki tatu baada ya ajali mbaya, safari za treni nchini Ugiriki wimeanza tena Jumatano Machi 22. Treni zimeanza kufanya kazi katika baadhi ya maeneo ya Athens, mji mkuu wa Ugiriki. Hizi ni treni za abiria zinazounganisha Piraeus, bandari kubwa karibu na Athens, hadi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Eleftherios Venizelos (kilomita 40 kutoka mji mkuu), zile za kati ya Athens na Chalkis (kilomita 80) na katika maeneo mengine mawili katika Peloponnese ya magharibi ambapo treni zlianza kuonekana tena mapema Jumatano asubuhi, kulingana na mamlaka ya Hellenic Train.

Hata hivyo, safarii kwenye eneo ambapo ajali ya treni mbili zilizogongana ilitokea mnamo Februari 28 hazitaanza tena hadi Aprili 1, kulingana na Waziri mpya wa Uchukuzi, Georges Gerapetritis. Ni njia kuu ya nchi hiyo, yenye urefu wa kilomita 600 na ambayo kuunganisha Athens hadi Thesaloniki, jiji la pili la Ugiriki, upande wa kaskazini. Waziri wiki iliyopita aliahidi hatua za ziada za usalama, ikiwa ni pamoja na madereva wawili kwenye treni za kati na "wasaidizi watatu badala ya wawili hadi sasa kwenye treni za abiria za Intercity kati ya Athens na Thessaloniki".

Serikali ya kihafidhina yanyooshewa kidole

Ikihusishwa hasa na makosa ya mkuu wa kituo aliyekuwa zamu jioni hiyo, ajali hii, mbaya zaidi ambayo Ugiriki imeshuhudia, pia imedhihirika kwamba kumekuwa na uzembe fulani kwa upande wa Serikali katika uboreshaji wa mifumo ya usalama ya treni ya kisasa. Usafiri wa reli nchini Ugiriki bado haujaendelezwa, unajumuisha tu karibu kilomita 2,100 za njia. 

Siku moja baada ya ajali hiyo, Waziri wa Uchukuzi Kostas Karamanlis alijiuzulu. Maandamano makubwa ya watu wenye hasira, mara nyingi yakiwa na vurugu, yametikisa Athens na miji mingine tangu ajali hiyo, yakinyooshea kidole serikali ya kihafidhina ya Kyriakos Mitsotakis lakini pia watangulizi wake wa mrengo wa kushoto kwa kupuuza usalama wa treni.

Kwa shinikizo, Kyriakos Mitsotakis alitangaza Jumanne jioni kwamba uchaguzi mkuu utafanyika mwezi Mei bila hata hivyo kutaja tarehe kamili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.