Pata taarifa kuu
USALAMA WA BARABARANI

Ajali ya treni Ugiriki: Mgomo na maandamano, hasira yatanda

Ghasia kati ya polisi na waandamanaji zimezuka tena nchini Ugiriki siku ya Jumatano Machi 8 huku hasira zikitanda baada ya ya ajali ya treni iliyosababisha vifo vya watu 57, huku wengine sasa wakiitaka serikali kujiuzulu.

Waandamanaji wakikabiliana na polisi wakati wa maandamano kufuatia ajali mbaya ya treni mbili kugongana uso kwa uso karibu na jiji la Larissa, Athens, Machi 8, 2023.
Waandamanaji wakikabiliana na polisi wakati wa maandamano kufuatia ajali mbaya ya treni mbili kugongana uso kwa uso karibu na jiji la Larissa, Athens, Machi 8, 2023. REUTERS - ALEXANDROS AVRAMIDIS
Matangazo ya kibiashara

Ajali hiyo ya treni, iliyotokea Februari 28, iliua watu 57, wengi wao wakiwa wanafunzi, na kuzua ghadhabu ya umma juu ya hali mbaya katika shirika la reli nchini Ugiriki.

Zaidi ya watu 65,000 wameonyesha ghadhabu zao Jumatano hii kote Ugiriki, wakati wa siku mpya ya maandamano yaliyogubikwa na mgomo kamili katika sekta ya umma na ya kibinafsi. Waandamanaji wanaamini kwamba miaka ya upuuzi, uwekezaji duni na uhaba wa wafanyakazi ndio chanzo cha janga hilo.

Huko Athens, zaidi ya watu 40,000, wakiwemo wafanyakazi katika sekta ya usafiri, wanafunzi na walimu, wameandamana katikati ya mji mkuu wakiimba “Wauaji! na "Sote tuko kwenye behewa moja".

Baada ya wiki moja tayari kumejawa na maandamano katika mji mkuu wa Ugiriki, ni umati kama huo ambao haujawahi kushuhudiwa tangu muongo mmoja wa mzozo wa kiuchuminchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.