Pata taarifa kuu

Mashambulizi ya Urusi yaua watu wanne Kyiv

Urusi  imerusha ndege zisizokuwa na rubani nchini Ukraine na kusababisha vifo vya watu wanne karibu na jiji kuu Kyiv, wakati rais wa China Xi Jinping akiondoka jijini Moscow baada ya ziara ya siku mbili. 

Wanajeshi wa Ukraine wakikabiliana na masamulizi ya Urusi.
Wanajeshi wa Ukraine wakikabiliana na masamulizi ya Urusi. © José Pedro Frazão/RFI
Matangazo ya kibiashara

Ukraine inasema imeangusha ndege zisizo na rubani 16 kati ya 21 zilizotengenezwa nchini Iran, zilizorushwa katika anga lake zikitokea nchini Urusi. 

Jijini Kiev, kituo cha elimu na majengo mawili, yanayotoa hifadhi kwa watu, yameshambuliwa, huku magari zaidia ya 20 yakiharibiwa. 

Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, ametembelea mji wa Bakhmut, ambako vita vimeendelea kupamba moto kati wanajeshi wa nchi yake na wale wa Urusi. 

Katika hatua nyingine, Waziri wa Mambo ya nje wa Uingereza James Cleverly, amesema hakuna silaha ya nyuklia zinatumiwa nchini Ukraine, baada ya Urusi kuishtumu kuwa inaipa msaada Kiev silaha hizo. 

Rais wa China Xi Jinping, akiwa ziarani jijini Moscow alisema nchi yake ilikuwa na mpango wa kuwa na suluhu ya mzozo wa Ukraine kwa njia ya amani, jambo ambalo Urusi imesema iko tayari kuithathmini. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.