Pata taarifa kuu

Papa Francis 'anamwomba' Vladimir Putin kukomesha vita nchini Ukraine

Kiongiozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis amehutubia waumini Jumapili, Oktoba 2 akimlenga moja kwa moja rais wa Urusi, akiomba kukomesha mzozo nchini Ukraine. Papa Francis pia amelaani unyakuzi wa hivi karibuni wa majimbo ya Urusi, na akamwomba Rais Zelensky aonyeshe uwazi "kwa mapendekezo madhubuti ya amani".

Papa Francis akiwabariki waumini mwisho wa sala ya adhuhuri ya Malaika wa Bwana, kutoka kwenye dirisha la studio yake linalotazamana na Uwanja wa Mtakatifu Petro, mjini Vatican, Jumapili, Oktoba 2, 2022.
Papa Francis akiwabariki waumini mwisho wa sala ya adhuhuri ya Malaika wa Bwana, kutoka kwenye dirisha la studio yake linalotazamana na Uwanja wa Mtakatifu Petro, mjini Vatican, Jumapili, Oktoba 2, 2022. AP Photo/Alessandra Tarantino
Matangazo ya kibiashara

Kama ishara ya wasiwasi mkubwa wa kuongezeka kwa mzozo nchini Ukraine, papa ametoa hotuba yake yote Jumapili kuhusiana na vita.

Papa Francis amesema "anahuzunishwa sana na mito ya damu na machozi yaliyomwagika katika miezi ya hivi karibuni".

Inasikitisha kwamba ulimwengu unajifunza kuhusu jiografia ya Ukraine kupitia majina kama Bucha, Irpin, Mariupol, Izium, Zaporizhia na maeneo mengine, ambayo yamekuwa mahali pa mateso na hofu isiyoelezeka.

Lakini kwa mara ya kwanza, Kiongozi wa kanisa Katoliki amezungumza moja kwa moja na hadharani akimlenga Vladimir Putin.

Wito wangu ninauwelekeza kwa Rais wa Urusi, nikimwomba, pia kwa upendo wa raia wake, kukomesha vurugu na vifo.

Francis, katika wito wake, pia amelaani vikali kitendo cha Urusi kunyakua majimbo ya Ukraine, "vitendo ambavyo ni kinyume na kanuni za sheria za kimataifa", hali ambayo, kulingana na papa, "inaongeza hatari ya kuongezeka kwa machafuko ya nyuklia, hadi kusababisha hofu ya athari zisizoweza kudhibitiwa na ya janga katika kiwango cha kimataifa."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.