Pata taarifa kuu

Moscow: Raia wa Ukraine waliopiga kura ya maoni wataka kuwa Warusi

Maafisa wa Urusi katika majimbo manne ya Ukraine, ambako kura ya maoni imekuwa ikifanyika kuanzia wiki iliyopita, wanadai kuwa raia wa Ukraine waliopiga kura wameamua kuwa, wanataka kuwa raia wa Urusi.

Kura ya maoni Donetsk katika jimbo la Donbass, Septemba 27, 2022.
Kura ya maoni Donetsk katika jimbo la Donbass, Septemba 27, 2022. AP
Matangazo ya kibiashara

Kura hiyo ya maoni ambayo imelaaniwa na Ukraine na Mataifa ya Magharibi, ilimalizika jana, katika kile kinachoonekana ni mpango wa Urusi kuchukua ardhi ya Ukraine, kama ilivyofanya mwaka 2014 ilipochukua jimbo la Crimea. 

Wakaazi wa Ukraine wanaoishi kwenye majimbo hayo manne yanayodhibitiwa na wanajeshi wa Urusi, ya of Donetsk , Luhansk, Kherson na Zaporizhzhia walionekana wakipiga kura hiyo iliyoandaliwa na serikali ya Moscow. 

Ripoti zinasema; hadi watu Milioni nne walishiriki kwenye kura hiyo ya maoani katika majimbo hayo manne, ambayo ni sawa na asilimia 15 ya êneo lote la Ukraine. 

Hatua hii ya Urusi inamaanisha kuwa, iwapo majimbo hayo manne yatashambuliwa na Ukraine katika siku zijazo, Moscow itadai kuwa ardhi yake imevamiwa. Wiki iliyopita rais Vladimir Putin alionya kuwa, yuko tayari kutumia silaha za nyuklia kulinda êneo la nchi yake. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.