Pata taarifa kuu

Urusi yakiri makosa katika harakati za kuhamasisha askari wa akiba kupigana nchini Ukraine

Serikali ya Urusi, imekiri kuwa makosa yalifanyika katika harakati zake, za kuwakusanya wanajeshi wa akiba kwenda kupigana nchini Ukraine , huku kukiwa na upinzani wa umma unaoongezeka. 

Katika picha hii iliyotengenezwa kutoka kwa video iliyotolewa na Huduma ya Habari ya rais wa Urusi, Rais wa Urusi Vladimir Putin akihutubia taifa huko Moscow, Urusi, Jumatano, Septemba 21, 2022.
Katika picha hii iliyotengenezwa kutoka kwa video iliyotolewa na Huduma ya Habari ya rais wa Urusi, Rais wa Urusi Vladimir Putin akihutubia taifa huko Moscow, Urusi, Jumatano, Septemba 21, 2022. AP
Matangazo ya kibiashara

Dmitry Peskov, msemaji wa rais Vladimir Putin amekiri kufanyika kwa makosa hayo lakini akatoa hakikisho la baadhi ya magavana kufanya juhudi kuhakikisha hali hiyo inarekebishwa. 

Aidha, ripotizinasema, watu wasio na uzoefu wa kijeshi au ambao ni wazee sana au walemavu, walitakiwa kujiunga na jeshi hilo la akiba, amri hii ya wiki iliyopita, ikisababisha maandamano makubwa nchini humo huku takriban watu elfu mbili wakizuiliwa. 

Baadhi ya wataalamu wa kijeshi wa nchi za magharibi na Ukraine, wanasema uamuzi wa rais Vladimir Putin, unaonyesha kuwa majeshi ya urusi yameshindwa vibaya katika uwanja wa vita nchini Ukraine, zaidi ya miezi saba baada ya Moscow kuanzisha uvamizi wake. 

Wakati hayo yakijiri, serikali ya Urusi inasema haijachukua uamuzi wa kufunga mipaka yake, ili kuzuia idadi kubwa ya wanaume wanaokimbia nchi hiyo, siku chache baada ya tangazo la kuwakusanya wapiganaji zaidi kwenda nchini Ukraine. 

Wakati hayo yakijiri, serikali ya Urusi inasema haijachukua uamuzi wa kufunga mipaka yake, ili kuzuia idadi kubwa ya wanaume wanaokimbia nchi hiyo, siku chache baada ya tangazo la kuwakusanya wapiganaji zaidi kwenda nchini Ukraine. 

Kifaa maalum kilichorushwa angani na watalaam wa masuala ya anga nchini Marekani NASA, kuona  iwapo kinaweza kugongana na sayari ya dunia, kimegonga  kitu kama jiwe karibu na jua. 

Kifaa hicho kilichopewa jina la DART kilienda umbali wa Kilomita Milioni 11 kutoka duniani, siku ya Jumatatu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.