Pata taarifa kuu

Maafisa wa tawala zinazounga mkono Urusi Volnovakha wasema wanatishiwa

Urusi imeanzisha leoIjumaa hii, Septemba 23 kura ya maoni katika mikoa minne ya Ukraine inayoyakalia kimabavu mashariki na kusini mwa Ukraine ili kuamua kama mikoa hiyo itaunganishwa na Urusi. 

Kura za kuunganishwa kwa maeneo ya Ukraine yanayokaliwa kimabavu na Urusi zitaanza Ijumaa hii, Septemba 23 katika mikoa minne ya Ukraine. Kwenye bango hili kuna maneno haya 'tunarejea nyumbani'.
Kura za kuunganishwa kwa maeneo ya Ukraine yanayokaliwa kimabavu na Urusi zitaanza Ijumaa hii, Septemba 23 katika mikoa minne ya Ukraine. Kwenye bango hili kuna maneno haya 'tunarejea nyumbani'. © Anissa el Jabri/RFI
Matangazo ya kibiashara

Ijumaa hii, Septemba 23 katika mikoa minne ya Ukraine. Maeneo hayo ambayo yako chini ya udhibiti kamili ya vikosi vya Urusi na vile vinavyounga mkono Urusi, pia sasa yote iko chini ya shinikizo la kijeshi kutoka Kyiv. 

Mikoa minne tayari imetangaza kuanza kwa zoezi la upigaji kura itakayofanyika kuanzia leo hadi Jumanne wiki ijayo katika mikoa minne ya Luhansk, Donetsk, Kherson na Zaporizhzhia, inayowakilisha karibu asilimia 15 ya ardhi ya Ukraine.

Katika maeneo yaliyotekwa hivi karibuni, mashambulizi mengi dhidi ya viongozi wa tawala zinazounga mkono Urusi yameripotiwa katika wiki za hivi karibuni. Katika maeneo ya Kherson Melitopol na Berdyansk kunaripotiwa vifo. 

Mamia kwa maelfu ya watu wataweza kupiga kura hadi Septemba 27. Mkoa wa Luhansk umetangaza kuwa raia ambao wamekimbilia Urusi wataweza kupiga kura wakiwa huko.

Huko Volnovakha, jiji kuu la kwanza lililochukuliwa wakati wa uvamizi wa vikosi vya Urusi na vile vinavyounga mkono Urusi, maafisa wengine wanazungumzia juu ya vitisho vinavyowakabili.

Kiongozi wa wanaotaka kujitenga na Ukraine huko Donetsk Denis Pushilin ameizungumzia siku hii kama muhimu na ya kihistoria na kusema huu ndio uhalisia wa sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.