Pata taarifa kuu

Ujerumani kuwa tayari kuwapokea wanajeshi wa Urusi wanaotoroka jeshi

Ujerumani iko tayari kuwapokea na kuwapa hifadhi wanajeshi wanaotoroka jeshi la Urusi "ambao wanatishiwa kukandamizwa vibaya", ametangaza Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani katika mahojiano yaliyochapishwa siku ya Alhamisi, siku moja baada ya tangazo la kuongezwa kwa askari wa akiba wa Urusi kupigana nchini Ukraine. 

Wanajeshi wenye silaha (wanaodaiwa kuwa wanajeshi wa Urusi) hutembea karibu na kambi ya kijeshi ya Perevalnoye mnamo Machi 13.
Wanajeshi wenye silaha (wanaodaiwa kuwa wanajeshi wa Urusi) hutembea karibu na kambi ya kijeshi ya Perevalnoye mnamo Machi 13. REUTERS/David Mdzinarishvili
Matangazo ya kibiashara

"Yeyote anayempinga Putin kwa ujasiri na hivyo kujiweka katika hatari kubwa anaweza kuomba hifadhi ya kisiasa nchini Ujerumani," amesema Nancy Faeser katika mahojiano haya na toleo la Jumapili la Gazeti la Frankfurter Allgemeine Zeitung, huku Waziri wa Sheria Marco Buschmann akisema kwenye ujumbe wa Twitter kwamba Warusi waliokimbia nchi yao wako tayari "kupokelewa".

Pendekezo hili linakuja siku moja baada ya tangazo la kuongezwa kwa idadi askari wa akiba wa Urusi kupigana nchini Ukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.