Pata taarifa kuu

Moscow yang'ang'ania kufanya kura za maoni kuunganishwa kwa maeneo inayokalia Ukraine

Licha ya shutuma nyingi za kimataifa na mapigano yanayoendelea, mamlaka za utawala za maeneo yaliyotekwa na Urusi zinaendelea na msimamo wao wa kufanya kura za maoni za kuunganishwa kwa maeneo  yao na Urusi, kura ambazo zimepangwa kufanyika siku ya Ijumaa.

Wanajeshi wa Urusi huko Kherson kusini mwa Ukraine, Ijumaa, Mei 20, 2022.
Wanajeshi wa Urusi huko Kherson kusini mwa Ukraine, Ijumaa, Mei 20, 2022. AP
Matangazo ya kibiashara

"Kura itaanza kesho na hakuna kitakachoweza kuizuia," Vladimir Salo, mkuu wa utawala wa uvamizi katika eneo la Kherson, kusini mwa nchi, ameonya kwenye televisheni ya Urusi. Mbali na mkoa wa Kherson, ule wa Luhansk, Donetsk na Zaporizha inahusishwa na kura ya maoni juu ya kuunganishwa kwa Urusi, ambapo matokeo yake, bila ya kushangaza, yatawezesha kuunganiswa kwa maeneo haya na Urusi.

Kura hizo za maoni zinazoelezwa kama "za ajabu" na jumuiya ya kimataifa, zitafanyika kwa muda wa siku nne, licha ya vita vinavyoendelea. Mamlaka inazounga mkono Urusi katika eneo la Donetsk pia imeeleza kuwa kura ya maoni itafanyika mbele ya nyumba katika kipindi cha siku tatu za kwanza, vituo vya kupigia kura havitafunguliwa hadi siku ya mwisho ya uchaguzi.

Wakati huo huo mapigano yanaendelea kwenye uwanja wa vita. Huko Zaporizhia, kulingana na viongozi wa eneo hilo, makombora tisa yalirushwa na jeshi la Urusi, na kuua angalau mtu mmoja. Kwa upande wao, wanaotaka kujitenga wameishutumu Ukraine kwa kutaka kuwatisha wananchi kabla ya kura ya maoni kwa kupiga risasi sokoni mjini Donetsk na kusababisha mlipuko katika soko la Melitopol. Madai ambayo yamekanuhwa na mamlaka ya Ukraine.

Katika hotuba yake Jumatano asubuhi, Vladimir Putin alitishia kutumia "njia zote muhimu" kulinda Urusi, ambayo inaweza kujumuisha maeneo ambayo yataunganishwa kufuatia kura hizi za maoni. Vitisho ambavyo rais wa Ukraine alisema "haviamini" na ambavyo vililaaniwa vikali na wakuu kadhaa wa nchi katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, akiwemo Rais wa Marekani Joe Biden na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.