Pata taarifa kuu

Putin anataka 'kuangamiza haki ya Ukraine kuwepo', Biden aiambia UN

Katika siku ya pili ya Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Rais wa Marekani Joe Biden ametoa hotuba kali dhidi ya Vladimir Putin na uvamizi wa Ukraine, Jumatano hii, Septemba 21, 2022 mjini New York.

Rais wa Marekani Joe Biden wakati wa hotuba yake mbele ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Septemba 21, 2022.
Rais wa Marekani Joe Biden wakati wa hotuba yake mbele ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Septemba 21, 2022. REUTERS - BRENDAN MCDERMID
Matangazo ya kibiashara

Joe Biden, wakati wa hotuba yake iliyoubiriwa katika jukwaa la Umoja wa Mataifa, hakuficha neno au kupoteza muda. Ameishutumu Urusi moja kwa moja kwa "kukiuka bila aibu" kanuni za msingi za Umoja wa Mataifa kwa kushambulia Ukraine, ameripoti mwandishi wetu huko New York, Carrie Nooten.

"Vita vya kikatili na visivyo vya lazima," amesema. Biden amesema, Vladimir Putin anataka tu "kuangamiza haki ya Ukraine kuwepo". "Mwanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa amevamia jirani yake, akitaka kufuta taifa huru kwenye ramani," almeongeza.

Popote unapoishi, chochote kile unachoamini, lazima ujitenge na kumwaga damu. Hii ndiyo sababu mataifa 141, kwenye Baraza Kuu, yalikusanyika na kwa kauli moja kukosoa vita vya Urusi dhidi ya Ukraine.

Kuhusu uzushi wa Urusi juu ya uwezekano wa utumiaji wa silaha za nyuklia, "haiwezekani kushinda vita vya nyuklia na haipaswi kuifanya", amebainisha Joe Biden, akitaja vitisho "vya kutowajibika".

Wakati huo huo, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, ambaye tayari amezungumza kwa ukali dhidi ya Urusi Jumanne, alitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa Jumatano "kuweka shinikizo kubwa" kwa Rais wa Urusi Vladimir Putin, ambaye alisema yuko tayari kutumia "kila njia." " katika safu yake ya ushambuliaji dhidi ya nchi za Magharibi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.