Pata taarifa kuu

Recep Tayyip Erdogan: Ninaami kwamba Putin ana nia ya kumaliza vita nchini Ukraine

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, amesema anaamini kuwa rais wa Urusi Vladimir Putin, anatafuta mbinu ya kumaliza vita alivyoanzisha nchini Ukraine, na hatua kubwa itachukuliwa. 

Vladimir Putin katika Kongamano la Uchumi la Mashariki huko Vladivostok mnamo Septemba 7, 2022.
Vladimir Putin katika Kongamano la Uchumi la Mashariki huko Vladivostok mnamo Septemba 7, 2022. AP - Sergei Bobylev
Matangazo ya kibiashara

Rais Erdogan amesema, kwa kuzingatia mazungumzo aliyokuwa nayo na kiongozi huyo wa Urusi, anapenda vita hivyo vimalizike haraka iwezekanavyo. 

Aidha, Erdogan amesema baada ya mazungumzo yake na Putin wiki iliyopita, vita vinavyoendelea nchini Ukraine vinaonekana kumsumbua. 

Kauli hii ya kiongozi huyo wa Uturuki, imekuja wakati huu Ukraine ikiendelea kuchukua baadhi ya maeneo Mashariki mwa nchi yake, iliyokuwa inashikiliwa na wanajeshi wa Urusi. 

Wakati hayo yakijiri, Kyiev  imeapa kuondoa vitisho kutoka Moscow  baada ya majimbo mawili yanayodhibitiwa na wanajeshi wa Urusi, kutangaza mpango wa kuwa na kura za maoni, kuwa sehemu ya Urusi wiki hii. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.