Pata taarifa kuu

Ukraine: Putin atangaza 'amri ya kuongeza idadi ya wanajeshi walio tayari kwa vita'

Rais wa Urusi Vladimir Putin ametangaza Jumatano Septemba 21 kwamba  ametia saini amri ya kuengeza idadi ya askari wa akiba kwa ajili ya "operesheni yake maalum ya kijeshi" nchini Ukraine, malengo ambayo amehakikisha kuwa hayajabadilika.

Katika picha hii iliyotengenezwa kutoka kwa video iliyotolewa na huduma ya vyombo vya habari ya rais wa Urusi, Rais Vladimir Putin anahutubia taifa mjini Moscow, Jumatano, Septemba 21, 2022.
Katika picha hii iliyotengenezwa kutoka kwa video iliyotolewa na huduma ya vyombo vya habari ya rais wa Urusi, Rais Vladimir Putin anahutubia taifa mjini Moscow, Jumatano, Septemba 21, 2022. AP
Matangazo ya kibiashara

 

Rais wa Urusi Vladimir Putin siku ya Jumatano ametangaza kuongeza idadi ya wanajeshi walio tayari kwa vita, na hivyo kufungua njia ya kuongezeka kwa mzozo nchini Ukraine. "Ninaona kuwa ni muhimu kuunga mkono pendekezo la [Wizara ya Ulinzi] la kuongeza sehemu ya askari wa akiba wale ambao tayari wamehudumu [...] na ambao wana uzoefu unaofaa," Putin amesema.

Rais Putin amesema kuwa nchi za Magharibi zimeonyesha kuwa lengo lake ni kuiangamiza Urusi na kwamba zimejaribu kuwageuza watu wa Ukraine kuingia kwenye vita kwa lazima.

Lengo letu ni kuikomboa Donbas, ameongeza.

Rais Putin anasema nchi za Magharibi zimeonyesha kuwa hazitaki amani kati ya Ukraine na Urusi.

Putin pia ametangaza kuwa kuanzia leo ni muhimu kuchukua uamuzi wa haraka ili kulinda watu katika ‘’ardhi zilizokombolewa’’.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.