Pata taarifa kuu

Ukraine bado yadhamiria kurejesha maeneo yake licha ya tangazo la Putin

Baada ya tangazo la Vladimir Putin la uhamasishaji wa sehemu ya askari wa akiba wa jeshi la Urusi, Ukraine imedhamiriwa kuendelea na operesheni yake kurejesha kwenye himaya yake maeneo yanayokaliwa na jeshi la Urusi.Β 

Mtu huyu akikanyaga bendera ya Urusi katika mji wa Kupiansk, mkoa wa Kharkiv, Ukraine, Septemba 19, 2022.
Mtu huyu akikanyaga bendera ya Urusi katika mji wa Kupiansk, mkoa wa Kharkiv, Ukraine, Septemba 19, 2022. via REUTERS - UKRAINIAN PRESIDENTIAL PRESS SER
Matangazo ya kibiashara

Huko Kyiv, maafisa na wachambuzi wanasema kwamba tangazo la Urusi linaonyesha jinsi gani Kremlin inaendelea kuwa na wasiwasi , lakini kwamba tangazo hilo halitakatisha tamaa serikali ya Ukrainekurejesha maeneo yake yanyokaliwa na jeshi la Urusi, wakati uwezekano wowote wa suluhisho la kidiplomasia sasa umekwama.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky bado hajatoa maoni yake kufuatia tangazo hili la Kremlin la kuwashirikisha katika vita dhidi ya Ukraine askari wa akiba 300,000, lakini watu wake waaminifutayari wameelezea hisia zao, wakitoa maoni yao juu ya tangazo hilo la Urusi kwenye mitandao ya kijamii.

Kwa ujumla, kwenye mitandao ya kijamii, Waukraine wanajibu kwa utulivu, bila hofu, na kwa dhamira, wakiwa na hakika kwamba jeshi lao lina uwezo wa kushinda mipango ya Kremlin.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.